Katika maisha yetu ya kila siku, kwa kujua au bila kujua inaweza kutokea mwenza/mpenzi wako, au rafiki au ndugu akatoa maneno kwako au kauli kwako (Huenda bila kukusudia) lakini ukajikuta kauli hiyo imekukera sana na kukusababishia hamaki na kuleta sintofahamu kati yenu.
Wakati mwingine aliyetoa kauli hiyo wala hajui kama amekukera, na huenda wala hakukusudia kukukera, ila kwako ni kama moto unafukuta moyoni mwako kwa hasira. Kauli hizi zinaweza kutafsiriwa kama kejeli, dharau, matusi, nk, ambazo kwako licha ya kukukera wakati mwingine zinachochea hasira inayosababisha wewe kutafuta mafanikio kwa hasira, kwa kuwa unahisi umekosewa na unataka kuthibitisha kwamba aliyetoa kauli hizo amekosea na wewe ni mtu bora kuliko wengi wanavyofikiri.
Miaka ya nyuma, mimi na mpezi wangu (wa wakati huo) tulikuwa tukigombana mara kwa mara, na ugomvi wetu kwa kiasi fulani ulisababishwa na kuwa na mitazamo tofauti kuhusu maisha, hivyo kupelekea ugomvi, hasira na wakati mwingine maneno makali kati yetu.
Siku moja mpenzi wangu huyo katikati ya ugomvi akapandisha sauti na kuniambia kwamba 'magomvi yote hata chanzo chake ni tofauti ya kiwango cha elimu kati yetu', akimaanisha kwamba yeye amesoma zaidi kuliko mimi ndio maana hatuelewani na kugombana mara kwa mara (Shabash!!)
Nikiri kwamba nilitaka kupasuka kwa hasira, kwa jinsi nilivyokereka kwa kauli na mtazamo ule. Kwa kiasi fulani ilichochea hisia za kusaka mafanikio na maendeleo kuthibitisha kwamba alichosema si cha kweli. Miaka mingi imepita sasa, lakini pamoja na kwamba baadaye tulikuja kuachana (Si kwa sababu ile) kauli yake imebaki kichwani mwangu na wala sijawahi kumwambia jinsi nilivyokerwa na kuumizwa na kauli ile.
Je, wewe yamekupata kama hayo? Uliwahi kupewa kauli yoyote iliyokukera? Na mwenza/mpenzi/rafiki au ndugu? Hebu tiririka ili nasi tujifunze kutoka kwako.