Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Walec

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2017
Posts
1,364
Reaction score
3,326
Wakuu mambo vipi, leo naomba tufanye kushare kila mtu jinsi alivyochomoka Nyumbani kwao.. Hii itatoa hamasa kwa wale waliokua nyumbani na kuogopa kuhama na kuanza kujitegemea.

Janga hili linawakumba wana vyuo wengi,unakuta mtu anamalza chuo akiwa labda ana 25 then anarud nyumbani, mbaya zaidi anasubir kazi, halafu kazi zenyewe haijulikani utapata lini.

Hii inapelekea wana wengi kua na fear ya kuchomoka home. Kiukwel hali ya kukaa hom inakata sana..Mzee unakuta anachomoka anakuachia mikazi flani hivi howcome.

Ukija upande wa MMU ndio mambo yanakua sio mambo, mtoto anataka aje kukusalmia unaona soo kwasababu upo nyumbani, inakata sana hii

Tukija kwenye maisha ya kujituma tu. Sometime unakosa hamasa ya kupambana kwasababu ugali wa bure, unalala bure, kila kitu bure. Hii inakua ngumu kuwaza kwa mapana ili kuanza kukamilisha dream zako..

Pia inakata sana. Pale wanao unakuta wapo na mageto yao. Lakini wewe kwako ni tofauti.

Sasa naomba kila mmoja aseme alichomokaje home na kuanza kukomaa na maisha..Achilia changamoto zake kikubwa hapa ni kusepa kwa maza.

Mimi binafsi gheto nilianza kukaa soon nilivyoingia chuo, nakumbuka nilipata room ya elfu 50 nikaanza nayo kibishi, nikanunua bed ya 150, 5 kwa 6, nikatafuta feni tu ya elf 35..si unajua joto la dar..nikaingia k.koo nikavuta subwoofer ya elf 75 tu, gheto bila mziki sio geto ni choo, kujicheki mfukoni boom likawa lishakata, basi nikaendelea kuishi geto hadi namaliza chuo gheto likawa limesheheni tu.

sasa baada ya kumalza chuo. Ndio nikarudi home ujinga niliofanya ni kurudi home na baadhi ya vitu niliviuza. Kasheshe ndio ipo saa hizi. wakuu home akili inalala, vibe yote hakuna, hapa ndio najichanga nichomoke tena nirud geto nianze kupambana. hope ndani ya huu mwaka nitakua nishasepa hom kwa mara nyingine.

Sasa share kitu basi nawewe.

Nini lilikusukuma usepe home?
Kitu gani kilikupa mzuka wa kuanza kukaa geto?
Vipi ulianza kukaa geto ukiwa na kazi au kibishi tu?

Maisha yalikuaje since day one?
Je ulienjoy uamuzi wako wa kusepa home?
ulianza kununa vitu gani vya msingi na kuanza kuishi geto
Una lipi la kuwaambia wana walioko home hadi leo wakiogopa kukaa geto kisa hawana ajira bado?

Karibuni wakuu.

images%20(2).jpeg

 
Daaaah nimekumbukaa mbali sana nimemaliza chuo 2015 nimesota mno 2016 nikajilipua nikatoka home kigambon mpaka tabata cna kaz uzur nilikuwa nakila kitu kuanzia godoro kitanda fen redio tv chumba 70k nikalipa six month pesa niliomba nikabakia na laki hiv piga mishe kitaa na laki ikakata maisha yakawa magum sana nikawa nafanya kaz yyte iliyopo mbele yangu nimebeba tofali nimeuza sabun lkn wap baada ya miez mitano nikarudisha mpira kwa kipa nikaenda home nikakaa miez mitano nikasepa tena nikaona nihame mkoa mpaka sasa niko arusha mi siiti gheto naita nyumba sahiv nipo nishazoea.
 
Back
Top Bottom