wakuu mimi nimemaliza chuo mwaka juzi (2019), kwa sasa nina miaka 29 nipo home bado, nimeangaika kutafuta kazi sijapata, nimesoma huu uzi nimeisi kama nimesha potea kwenye maisha, naombeni mbinu na mimi nichomoke hapa home nikapange wakuu??
Kaka umefanya nimejisikia vibaya sana sana sana!
Kuna kitu kimejijenga kwenye vichwa vya watu kua kupanga geto kwa kijana ni LAZIMA!
Jibu ni hapana!!!!!!!!!!!!
Panga geto ikiwa unaona ukiwa nyumbani akiri haitanuki
Ila sio razima ufanye hayo
Unakuta mtu amepanga room ila anapata hera
Analipa kod
Maji
Umeme na kula yeye ila hakuna serving! Hiyo ni sawa sawa na nothing!!!!!
Wew usijutie kua nyumbani ,labda kuwe na sababu MUHIMU ...
Tafuta kaz YEYOTE HALALI! kisha komaa kuzifanya
Iwe kubeba mawe
Iwe kusaidia kujenga
Iwe kusogeza spea
Iwe chochote
Iwe kuzibua mitaro
Iwe kuzibua vyoo
Iwe kuzoa taka
Iwe yeyote ile ifanye
Nenda hata ukawe condakta(nlikua condakta pia)
(Muda mwingine inabidi uvae uhusika wa watu wengine)
My brother mim ninae kuandikia na u boy wangu wa 25year lakin nlisha taka anza kukaanga viazi
Au kuuza UJI![emoji23][emoji23][emoji23] mim nnachekaa ila wew usicheke soma kwa makini
Kisha angalia utapata kiasi gan cha pesa kisha ki sev yaani ifanye hiyo pesa sio yako!
Baada ya muda utakua na pesa nyingi kiasi kisha hizo zitumie hizo kufungua biashara yeyote ile(nnaamin utaipa nidhamu sababu umehangaika kuipata hiyo pesa)
After hapo unaweza kupanga room au kujenga yakwako
Kupanga geto ni swala jema ikiwa unahitaji utanuzi wa akiri nje ya box
Ila sio lazima ikiwa mazingira yanakukataa
(Uhuru unaghalama zake!!!)