Ulianzaje kukaa gheto?

Nilianza kukaa ghetto nikiwa full na kila kitu, maana shule ilinishinda kutokana na mazingira ya home, hivyo nilianza mishe punde tu nilipomaliza four, nilikuwa na kitanda, sofa meza feni bila kusahau pasi, maisha ya ghetto yamenifunza mengi mno hasahasa uvumilivu na kupambana, nashukuru mungu nikijaliwa uhai mwezi ujao wa kumi mwishoni nahamia kwangu kimara
 
Hongera sana mkuu...ulipambana sana
 
Nilianza kukaa geto na mshikaji nikiwa first year ila nikajikataa nikakaa mwenyewe, hadi leo naishi mwenyewe...maisha ya kujitegemea yana changamoto sana.
Misosi ya kuunga, kula mpakani na mengine mazuri na mabaya, Inshort ukijitegemea akili inafunguka ukikaa home unabweteka na unakua huna 'freedom' na 'privacy'.
 
Broh samahan, km hutojari naomba uanzishe uzi wa hii stori yako kuna kitu cha kujifunza
 
Wewe jamaa kifipi una NGEKEWA....barikiwa sana
 
Ni kwel mkuu..challenge zipo..ila ndio akil inakaa sawa...
 
Mimi nilipomaliza tu chuo nikapata sehemu ya kujitolea wakawa wananipa hela kidogo nilikuwa nakaa home ila sikuweza kununua kitu nawakati nakula bure hela naenda tu saluni
Siku nilipochoka kujitolea nikaondoka na home nikawa nakaa na rafiki angu tunashare kodi na nilikuwa sina kaz lakini niliweza kununua vitu vingi tu
 
Aah umetisha sana......Hapa ndo naona ukikaa geto unakua na akili ya maisha..big up sana
 
Natamani kukaaaa ghetto na mm nianze ku experience life la kujipikia ila tatzo japa nakaa kwa Ndugu ana bonge la nyumbaaaa afuu vyumba vingine vipo empty aseeeee muda mwingne naachiwaga home nzima











but still university student hapa kwa Baba kegan.





but next year lazima kieleweke.
 
dah siiti getto saivi napaheshimu sana!!
ilikua baada ya kumaliza chuo.. niliumiza kichwa sana ntafanyaje nikae home.. hapana nitadharaulika sana.. kuna mshkaji mmoja nilisoma nae premary alikua mwanza anapiga mishe zake za boda boda.. nikaongea nae jamaa fresh.. nikatoka home bila kuwaanbia naenda mwanza.. ilibd niwadanganye maana wasingeruhusu niondoke bila hela... nilikaa kwa mshakaji mpk kesho ananiheshim sana.. nilikua nalala kwenye sofa.. usiku jamaa anakuja kalewa kinoma.. anankuta macho inabidi nitoke amgonge dem wake.. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ (nimepigwa exile sana).. ikawa kidogo tabu kupata kazi ya taaluma yangu.. nikaamua kushika chaki.. nikafundisha fizikia na hesabu.. nikawa nalipwa vizur.. mshahara wa kwanza tuu.. nikahama na kununua kitanda. mshahara wa pili nikaanza kununua vitu vingne.. nilikua na jeuri sana.. maana nilikua sinunui kitu cha kawaida.. yaan najibana miezi mitatu.. then naenda nunua bonge la kabatii.. nikilileta geto nasema sinunui tena kabati maisha yangu yote.. lbd anunue mwanamke.. saiv nikimkaribisha dem geto lazm aulize umeoa!?? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimejifunza mengi sana.. hapa ni nyumbani si geto tena!!
 
Unaweza sepa hata ukiua chuo..ila kama unataka life ya kujitegemea mapema..we sepa tu
 
Hahaha daah..exile znauma mkuu...hilo swala la kununua kitu cha maana nalipenda sana...umetisha kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…