Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Mwaka wa 2 huu Ghetto! Nashukuru Mungu sina dalili ya kurudisha mpira kwa kipa(home). Naenjoy kupika chochote nnachopenda na kuamua mimi, mfano this weekend nimegoogle jinsi ya kupika kuku kama KFC vile nataka nijaribu nione😂😂😂 raha sana.

Kuna siku niliamka sina pesa kabisa aisee nikatafuta kila sehemu nilipowekaga hata coins sehemu zote kabatini uvunguni dah nikapata nikanunua zangu mihogo kachumbari mixer pepsi maisha yakaendelea😂😂. Na hiyo siku mother house naye akanikumbusha kulipa maji na umeme nikachoka kabisa.
Hongera sana jirani yangu
 
Nimehama toka vyumba viwili hadi single self
20210910_082855.jpg
20210910_082931.jpg
 
Miaka Ile AHM akiwa kashika usukani nilihama kutoka kwa mzee nikahamia kwangu. Nilikua na kitanda, godoro, shuka mbili, neti, jiko la mchina, sufuria tatu, ndoo mbili moja kuogea, moja maji ya kunywa, kabati sahani kijiko na kikombe.
Nyumba za kiswahili korido Kati chumba tatu kulia tatu kushoto. Mbele Baraza uani vyoo bafu jiko.
Nimehamia tu sijakaa sawa binti wa mwenye nyumba kanifuata bombani nikichukua maji nikaoge na kuniambia
KAKA USIFUNGE MLANGO USIKU NITAKUJA . Aroo sijatongoza hata jina sijamuuliza.
Kweli bwana kwenye saa sita nasikia mlango unasukumba na mtu huyu ndani ya neti Tena amenyoa.....
Hii peleka kwenye kula tunda kimasikhara[emoji23]
 
Let me ask for my friend,

Kwao wana nyumba ya urithi na wazazi hawapo na inahitaji marekebisho mengi na watoto wapo zaidi ya mmoja ila wanaokaa hapo ni wawili tu yeye na sister ake.

Je ni bora akapange gheto au arekebishe nyumba yao akae hapo hapo ? Na kufanya marekebisho makubwa huku amepanga ni changamoto maana kwenye kupanga ataanza upya vitu vingi.

Faida ya kukaa hapo kwao ni gharama hazitakuwa kubwa za kodi kila mwaka, lakini hasara hana uhuru as wanafamilia wanaweza kuja saa yoyote.

Mna mshauri nini mtu wa aina hii wadau wa maghetoni[emoji1320][emoji1320]?
Ahame hapo,nyumbani ni nyumbani tu hata kama unaishi peke yako.
 
Back
Top Bottom