Ulianzaje kukaa gheto?

Mara umeanza Chuo, Mara evening class, Mara Boom
Story Haina Coordination, haiungiki
 
Mnaokaaa gheto au hata hizi nyumba zenye vyumba tofauti mnazoshare jiko, seble etc hebu elezeeni changamoto mnazokutana nazo,

Nilienda home kidogo nikaacha vitu vyote gheto nyumba tunashare wawili kupunguza costs, wakati nimeondoka jamaa angu kuna ndg yake akaja akawa analala chumbani kwangu maana sikuwepo... alivyokuwa anaondoka kuna vitu si akavipenda akaamue afanye shopping... kabeba viatu, suruali zangu pendwa, narudi hamna baadhi ya vitu
 
Kuna Muda inabidi ukubali kushuka chini ili uanze upya......

Miezi 2 kabla sijamaliza chuo miaka kadhaa iliyopita, nilikaa nikawaza hatma yangu. Unajua kuna ile ukiwa chuo familia inajibana na kukupa kila unachohitaji kwa kadri ya uwezo wao ili tu uishi vizuri. Ndivyo ilivyokuwa kwangu mimi. Familia ilinisapoti kwenye swala la kodi na nilikuwa naishi vizuri sana maeneo ya Mwenge.

Sasa miezi 2 kabla sijamaliza chuo nikakaa nikawaza, hivi hapa nikimaliza chuo nirudi tena home?....Hapana haitawezekana. Niendelee kukaa mwenge?...Hapana sitaweza kumudu gharama za maisha ikizingatiwa kuwa sikutaka kusumbua familia kuhusu maswala ya kodi n.k....Wamenisapoti vya kutosha toka primary hadi chuo. Uamuzi uliokuwepo ni kupambana mwenyewe...

Baada ya kumaliza chuo nikakaa mwenge kama mwezi mmoja kumalizia kodi yangu ambayo gharama ya pale ilikuwa 150k kwa mwezi...Nikahama nikahamia river side ndani ndani huko chumba cha 20k kwa mwezi. Ilikuwa ni new experience kwangu ikizingatiwa nimetoka kuishi ushuani kwa miaka 2 mfululizo pale mwenge...getto kali, choo ndani na mazingira mazuri sasa leo naenda kukaa sehemu ambayo choo tunapanga foleni na uswahili wa kila aina...Kwakuwa nilishaweka nadhir kuwa sirudi kwa kipa hata iweje, ikabidi nikomae....

Pale riverside nililipia miezi 6 ambayo ni kama 120k hela niliyoipata kwenye kusave na kujibana kipindi niko chuo. Ila nilikaa pale miezi 3 tu. Kwasababu sikuwa na kazi yoyote ya kuniingizia kipato...nimepambana sana kusaka mishe za pale mtaani lakini bado hali ikawa tete...Kichwa kikawa kinawaka moto sasa hii kodi ikiisha naishije tena. Frankly speaking, nilikuwa kila nikiwaza miezi 6 ijayo sioni kitu....nilikuwa sioni future ila kitu pekee ambacho hakikuisha akilini mwangu ni Hope. Nilijua tu hii ni transition period na siku moja nitasimama.

Baada ya mishe zangu kukwama yaani kila siku natumia hela siingizi, nikaona pale mtaani hapanifai. Nikafunga safari hadi magomeni kwa uncle wangu mmoja. Hapo nauli ya kurudi home kwa bimkubwa ni 400 tu ila sikutaka hata kupasikia. Nirudi kufanya nini sasa? Kula bure huku nikitia huruma?....Hapana.

Nimefika kwa uncle nikamwambia mzee mimi kiukweli ngoma ngumu. Hapa nilipo nimetoka Riverside kule nimeacha vyombo vyangu na kodi ya miezi 3. Sikuwa nimehama riverside ila tu nilifunga mlango na kusepa magomeni. Kwahiyo vyombo vyangu vilikuwa bado kule na kodi yangu ya miezi 3.
Uongo dhambi, pale kwa uncle nilifata uhakika wa kula tu 😁😁 manake kule riverside nilikuwa kila siku natumia hela sasa nikaona bora niende kwa uncle ambako nitakuwa na uhakika wa kula afu zile chenji ninazopata kwenye husstle zangu nazitunza.

Yes, dunia ikafunguka, nikajichanganya mtaani...piga sana kazi na fundi umeme site....somba sana maji magomeni kwenye mkokoteni kuwauzia wadau. Lengo lilikuwa moja ni kusepa kwa uncle.

Baada ya miezi 3 kuisha (means kodi yangu kule ya miezi 6 imekata), nikaenda riverside kuchukua tuvyombo twangu...nikaja nikatupaki kwa uncle...hapo nimapambana sana, weka akiba sana huku na huku, baada ya miezi 5 nikamuaga uncle...nikamwambia naenda kupanga....hapo sijasimama vizuri ila nikasema nitaweza. Na nilipanga pale pale magomeni jirani na uncle...hii ndiyo siku nilihama kwenye toroli a.k.a mkokoteni maana vyombo ni kitanda na godoro tu πŸ˜„πŸ˜„

Nakumbuka nikalipia chumba cha 50k nikaanza kuishi...husstle zikaendelea, nikanunua tv, radio, sofa na vitu vingine muhimu...

Kufupisha story....Leo na jana ni tofauti. Mungu ni mwema maisha yangu ni ndoto za vijana wengine japo sijafika....na nimeweza kumiliki getto kali tena kama lile la mwenge.

NB: kuna muda inabidi tukubali kushuka chini kutokana na uhalisi wa maisha. Ila baada ya muda tukikaza tutarudi juu....

Heshima na upendo mwingi sana kwa uncle wangu wa magomeni....saluti nyingi sana kwa mafundi umeme na wateja wangu wote wa maji magomeni....Those people treated me fairly and am always grateful.

Baadae nilikuja kubahatika kupata ajira na maisha yakaendelea....Ila never lose hope....Confort zone ni adui wetu...I wish the best to everyone working hard to live their dream.....Alhamdullilah

FOHADI.......Focus, Hardwork and Discpline.
 
Umeniispaya sana....kudos bro
 

Mkuu picha la ghetto hatupati?
 
Sasa kwanini hukufunga mlango wako!?
 
Mkuu picha la ghetto hatupati?
Sorry mkuu...sitaweza kulitupia picha la getto out of Privacy...I wish to continue being anonymous....kuna watu nawajua, wananijua, tunajuana na tunafahamiana sana wapo humu....so sitaki ku reveal Identity yangu....

Ila binafsi nafafijika na nimeridhika kila nikiliona...ngoja nikupe lugha ga picha...It is a self room...ina kila kitu muhimu kwa kijana....ila changamoto moja tu kupika ndo inshu hapa namsubili cocastic anifundishe.

PS: Nilipokuwa nauza maji...kuna mtu pengine anaweza jiuliza how a graduate...na mimi sitaki ku exaggerate story...ilikuwa ni kwamba....

Baada ya kuhamia magomeni, jirani na uncle alikuwepo kijana mmoja ambae tulizoeana sana...yule jamaa alikuwa anauza maji kwenye mkokoteni...Yaani kuna maboss alikuwa anawasambazia...sasa ilikuwa mimi namsindikiza kusukuma hayo maji....na sometimes akipata oder amechoka au alikuwa ananifanyia fair tu anasema wapelekee hayo maji then hela nachukua mimi...

Mkokoteni tunabeba dumu 10...na kila dumu 200 afu tulipokuwa tunachota ni free...so ukipiga trip tatu pale una buku 6. That is how it was.

NB: Nilihaso ndio ila nasema ukweli kabisa kama ningekuwa home kwa bimkubwa nisingeweza kusukuma maji kule.....Mi ni aina ya wale watu ambao tuko affected na ile WATANIONAJE?

so niliamua kwenda migomigo kwa sababu kule mimi ni mgeni na hakuna mtu ananijua so ile aibu sikuwa nayo. Ndio maana nikawa napushi maji na kupiga mishe zingine nyingi tu za halali...siwezi kuelezea kila kitu.

Ila inawezekana viongozi...na kwa mara ya kwanza wakati nakutana na huu uzi, nilikuwa bado naishi kwa uncle baada ya kufunga getto kule riverside. Nikawa inspired sana na hii thread.

Nimeijua JF kwa muda mrefu sana ila maamuzi ya kujiunga na JF 2020 ilikuwa baada ya kukutana na huu uzi na kuwa inspired..

Mr. Walec popote ulipo....wewe ni zaidi ya RikiBoy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…