Ukianza kukaa geto vitu Gani ni muhimu kuwa navyo?
Ukitaka kujua vitu muhimu vya kuanza navyo tumia formula hii kufikiria daily routine then vitu utavijua chap
Kila kimoja ntakipa namba yake
Let's gooo..
Ukiamka asubuhi(kabla ya kuamka ulilala ulilala wapi?si kitandani [emoji23][emoji23]
So unahitaji kitanda,neti na mashuka yake(1)
Haya tuendelee ukishaamka asubuhi utaenda kuoga,sasa utaogaje bila ndoo na kopo?labda kama kuna bomba la mvua bafuni [emoji23] ila kama hamna unahitaji ndoo.sasa hayo maji ya kuoga utayatoa wapi? Si Kwenye dumu la maji
So unahitaji ndoo na madumu ya maji kuhifadhi maji(2)
Ukishaoga utarudi zako ndani kuvaa nguo sasa utavaaje nguo bila kupiga pasi ??acha ushamba [emoji23] kuwa smart bhana
So unahitaji pasi ongezea na extension cable hapo au utachomeka pasi ukutani upigwe shoti ufe (3)[emoji23][emoji23]
Ukishavaa nguo zako baada ya kupiga pasi si utahitaji kula breakfast either ukanunue mihogo kwa mama ashura au ule kiporo cha ubwabwa cha jana usiku sasa hicho kiporo ulikiweka wapi? si Kwenye vyombo mjomba [emoji23][emoji23] utakulaje bila vyombo si utatumia sahani,mabakuli na masufuria na vikombe na vijiko(4)
Halafu kijana haupo serious hicho kiporo unadhani kilishuka kimiujiza kutoka mbinguni si ulitumia jiko kupika[emoji23](5) jiko la gesi ndo zuri kigheto ghetto chap kwa haraka
Sasa ukishakula si utatoka kwenda Kwenye mishe zako bro ghetto kumbuka haujaweka mapazia watu watachungulia ndani[emoji23](6) weka pazia bhana for privacy
Sasa si umeenda Kwenye mishe zako baadae ukirudi ghetto usiku
Utakua umechoka utaenda kuoga maji si yapo Kwenye madumu[emoji23][emoji23] chukua ndoo kaoge
Ukishaoga si utakua na njaa utatumia jiko na vyombo kupika utakula utashiba
Sasa ukishashiba nini kinafuata? si kulala
[emoji23]
Kitanda neti na mashuka si yapo haya kalale[emoji23][emoji23]
Afu kabla hujalala weka simu charge,extension cable si ipo bhana
Sema dah ongeza na feni mjomba si unajua joto Kali (7)
Mpaka hapo umeshajua vitu muhimu vya kuanza navyo yani unapoamka mpaka unapoenda kulala umevitumia ni hivo
1:kitanda neti na mashuka
2:ndoo na madumu ya maji
3
😛asi na extension cable
4:Vyombo
5:Jiko
6
😛azia
7:Feni
Game over.....
Vingine vya ziada
Tv, subwoofer, sofa,coffee table,fridge,kabati..
Nawasilisha.