Ulianzaje kukaa gheto?

Kama vipi wakugawie funguo ya geti kama wanaona shida kukufungulia,

Hapo sio pahala pa kuishi,unaweza fukuzwa na vibaka kukimbilia nyumbani pamefungwa na usipate msaada.
Kuna siku nimerudi kama mida ya saa 2 hivi,hapo jana yake walifunga geti,niligonga lakini hawakufungua..niliporudi nikaingia geto,nikasema ngoja niende Kwa mama ntilie nikapige msosi,Kuna dada alikuwa yupo jikoni anakula na mtoto wake,kutokana na uoga wa kufungiwa,nikamuaga kabisa nikamwambia naenda kula narudi si mda mrefu geti wasifunge..hee baadae narudi geti wamefunga,goooonga mlango lakini wapi..kitu kibaya zaidi sisi woote wapangaji,mwenye nyumba hayupo
 
Wanakufanyia kusudi,hama baadhi ya wamama wana roho mbaya
 
samahani mkuu ni geti kubwa au unaishi nyumba zile zenye vyumba vya ndani halafu kunakuwa na mlango mkubwa?

ni mkoa gani upo?
 
Hama hapo mzee [emoji23]
 

uko sawa mkuu wala hujakosea kuna wana miyeyusho sana ... kuna jamaa yangu nilimpa hifadh gheto daah aisee nilijuta sana
 
Kwani kipindi unapanga hukuwapa muongozo wa mida yako ya kurudi kwako,mimi geto kwangu narudi mda wowote tofauti na hapo mwenye nyumba atanirudishia pesa yangu
 
Kwani kipindi unapanga hukuwapa muongozo wa mida yako ya kurudi kwako,mimi geto kwangu narudi mda wowote tofauti na hapo mwenye nyumba atanirudishia pesa yangu
Mi nilifeli mwanzoni,mazingira Yale ya get kali niliyaona ila nikapuuzia..hapo ndo nilipobugi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…