Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Wakuu nina mengi ya kusimulia jamvini ttzo mwandiko mbovu,, nitaeleza Kwa kufupisha,,,,
Ukiamini Mungu na kuishi kwa Imani huku ukijituma Kwa nguv zote baraka utaziona.

Nilipo yaanza maisha rasimi baada ya kumaliza masomo yangu, safari yangu ilianzia Dodoma, sina ndugu nilifikia Kwa Wana walionitangulia kumaliza nashkuru walinipokea vzr tukaishi japokuwa baadhi ya changamoto nilipitia zisizo na maumivu kwani nilikua napata wakt mgumu pale mwana akija demu wake kitu ambacho kilitia uchachu wa kufight nikapange kwangu.

Nilitoka mbali na home wazaz wakiwa hawataki ila vile nilkua nishajiapia baada ya kumaliza chuo lazima nitoke mbali na home Kwa ajili ya kutafuta maisha,, nilifanya kama nilivyojipangia tangu nasoma,, wakati nakalibia kumaliza chuo miezi ya mwishoni mpenz wangu alibeba ujauzito wangu ikawa mkazo wa me kuwa mbali.
Mama mtu akabless me kutoka Kwa ajili ya kutafuta ili tuje tuishi wote. Nimeseto Kwa Wana Kwa miez 4 muda huo najitafuta katika ofsi flan hapa dodoma.
Mpka Sasa naandika ushuhuda huu nipo kwangu nilipo panga naishi na Mke wangu pamoja na mtoto wetu, life liko good kiasi Kila hitaji tunapata, kwa uweza wa M/Mungu mwakani tunahamia kwetu.
Nilicho jifunza kwenye maisha usiogope mtangulize Mungu katika kila jambo lako fanya kazi Kwa bidii mmbo yanajipa yenyewe,,,, zingatio Kwa sisi vijana wanawake Wana nguvu kubwa sana haswa ukimpata ambaye anajielewa na aliyetayari kufanya maisha katika kila hali.

Vilivyo Anza mpaka now,,, vijana tusikate tamaa Mungu sio wa kabila moja. View attachment 2389183View attachment 2389186View attachment 2389196View attachment 2389197View attachment 2389199View attachment 2389204
Safi sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom