Ulianzaje kukaa gheto?

Soon naingia gheto rasmi, 2 months from now

Nimeandaa bajeti ya 1.4M
Wakulungwa nipangilieni kwa kiasi hiko nakamilishaje room iwe full kbs, je inatosha au napaswa niongeze? Kama haitoshi kwa bajeti hiyo naweza kamilisha vitu gani

Nb/Ni chumba na sebule pia usipigie hesabu ya kodi

Kwenu wakulungwa nawasilisha[emoji1545][emoji1545]
 
Duuuj 1.4m gheto tu! Wewe ni wakishua aisee.
Huongera sana.
 
Inatosha sana

Nakadiria tu bei sio exact price lakini ina range humo humo

Kitanda na godoro around 300k
Feni 120k
Jiko la gesi mtungi mdogo 55k
Kitchen cabinet 100k
Tv 300k
Sabufa 100k
Mapazia,mashuka 80k
Pasi 35k
Extension cable 10k
Ndoo za maji
Fridge dogo 150k


Total 1,170,000/=

Inabaki 230,000/= ya misosi

Mchele
Unga
Mafuta ya kupikia etc
 
Vitu vilivyopanda bei, hapo vingiii anakosaaa,
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kitchen cabinets ipi laki? Akat kuanzua 150k uwiiii

Hiyo helaa kwa kuitaja nyingi, ingia kwa matumizi uone sasa,

Labda atanunua sio dukani. Kwa mtu yaan used.
 
Jiko la gesi chukua kopa gesi nahamini iyo ela unapata jiko la ges na chenchi inabaki
 
Kitchen cabinet ya milango miwili anapata kwa 100k tena wengine hadi 80k wanakuuzia mimi mwenyewe nipo kwenye process ya kununua soon tu

Hiyo ya 150k unayosemea wewe ni ya milango mitatu



Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…