Ulianzaje kukaa gheto?

Miqka hiyoooo Nilipomaliza chuo wakati nasubiria ajira nikapata tempo shirika fulani hivi private. .nikataka kwenda kupanga nianze maisha yangu. . Older Sista akanikatalia eti nitokee tu hom kwenda kazini Kwani haoni sababu ya mimi kutoka nyumbani.

Badae nikapata ajira serikalini uzuri nilikua na vijisenti kidogo nikanunua godoro la 5*6 sister akanipa gesi ndogo ilikuepo kwake nikaenda kuanzia maisha kulala chini.

Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilipangaga chumba huku nikiwa sina hela ya kununua kitanda, basi kila siku nikawa nazuga kama nampigia fundi seremala ili tu majirani wasikie "fundi unataka mbavu zote zisagike na sakafu ndugu yangu, hicho kitanda kinakamilika lini, kitanda kimoja unatengeneza mwaka mzima ndugu?

Maisha yalienda mdogo mdogo huko mbele nikapata pesa nikanunua kitanda na godoro kwa mpigo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha et mbavu zisagike na sakafu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haha unajiongelesha mwenyew kusaka excuse kwa majiran[emoji16][emoji16]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] we ni balaa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nilipo maliza form six niliingia kitaa ile direct from school hapo nilikuwa na elfu 10 nimeuza scientific calculator yangu home mother ana chumba kimoja amepanga. Ila mzee alikuwa ana nyumba mkoa mwingine wameshatengana hivyo niliamua nikomae nimsaidie mother.

Nililipa chumba 5,000 mwezi 1(miaka ya 2003 Tabora mjini, mtaa wa Bachu) nikabakiwa na hela ndogo ya kutumia. Nilianza kujichanganya kutafuta shule ya msingi nikafungua tuition center. Nikajitangaza mashuleni na masomo ninayofundisha, Mara madogo wakaanza kuwasili huku nimesambaza barua za ajira kuomba temporary job mashule ya pale mjini.

Kidogo nikaitwa kwenye interview shule moja pale jirani. Nikashangaa nimeitwa nimejazishwa mkataba wa miaka 2 matazamio miezi 6 nikashukuru Mungu nimepata uhakika sasa nmeanza lipwa mshahara kabisa. Sikurudi nyuma mpaka leo, mwaka ulipoisha zikatoka nafasi za induction teachers wiki 2 nikarudi nikaingia government nikawalipa ile shule ya private mshahara wao wa mwezi kuvunja mkataba wao nikaingia government school.

Baadae nikaomba kwenda chuo Udsm nikitokea kazini na mshahara juu. Mbele kwa mbele hadi leo nabadili machaka tu.
 
Asante sana Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…