Ulianzaje kukaa gheto?

Mkuu kwanza hongera kwa kuanza na vitu...

Ukishatoka hapo ndio utajua mishe ya kufanya coz utakua huna budi.. lakin ukiwa hom bado utaona huon mishe ya kufanyia hyo hela yako
 
Kodi hata miezi mitatu unaanzia
 
Nakumbuka baada ya masomo yangu niliishi kwa rafiki yangu kwa miezi mitatu nikisakanya kazi. Nilifanikiwa kupata kazi ya muda katika VTC moja! Mshahara wangu wa kwanza nilinunua godoro na kulipia chumba kwa miezi mitatu nikaamua kutoka kwa rafiki yangu japo alinisihii niendelee kukaa pale ili nijiimarishe zaidi. Nilihitaji uhuru wangu hivyo nikaamia geto kwangu. Nikatandaza maboksi chini nikaweka godoro langu la 5x6 maisha yakaendelea! Nilikuwa nina vikombe viwili, glass mbili, na jiko la mchina! Maisha yalienda!
 
Mimi moja ya shauku yangu kubwa ni kupanga ñdo first priority kwa sasa natarajia next year Mungu akijalia nitakuja hapa kuleta mrejesho wapi nilipo fikia najua haitakuwa Kazi rahis lkn Nia dhamira na shauku ninayo


Lengo langu ni hivi kuanzia sasa naanza kununua mazaga kidogo kidogo ya kigheto kama kuchonga kitanda , kununua godoro meza gesi navikusanya taratibu kabati mdogo mdogo ili kupunguza mzigo



This is my time 24 years old

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah nmetoka mbali sana, ishu ilikua uoga tu wa maisha ila nilichomoka kutoka kwenye mikono ya uncle hapo home ni mkoani, unajua unakula kwa kuamkiaa., asbh utaamka uoshe vyombo ilimradi usionekane mzgo na aunty yangu alikuwa mnoko sana maneno mengi mara kurud home mwisho sa1 usiku daah, ukichelewa kula hakuna kula,, uncle yangu nae alikuwa maneno mengi., nkaona sio kesi nkaanza jipanga mdo mdo, ghafla nkapata mchongo nkawa silipwi zaid ya kupewa 200k ya nauli na kula ofisini. Baada ya kupata mchongo maneno yalikuwa mengi sana hapa home nilikua najituma sana job narud usiku home nikichelewa wanamind yan daah kumbe me najipanga taratibu ili nisepe, aisee kukaa na ndugu kuna hitaji moyo sana.

Nilivyopata kodi tu nikaaga nimepata safar kumbe me ndo kibati.. nilianza na kulala chini na godoro lkn now nimepanga na sebule kabsa namiliki asset zote mhm.

Usiogope kujaribu ukipanga akili ya kupambana inakuja na michongo inatokea, ukifika 25yrs usikubali kukaa nyumbani pambana ingia kapange upambane na maisha huo ndo uanaume.
 

Kitanda acha kwanza, hapo muhimu godoro kwanza, gas na tuvyombo kdg tafuta kodi anza maisha
 
Umeniispire kinoum Sana mkuu kikubwa ni kuondoa Hofu kujiamini na kujituma mwakan naleta mrejesho wapi nilipofikia

Big up saan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana mkuu...Tunasubr mrejesho..Mungu akutangulie
 
Hongera sana mkuu...sasa vp anko ulirud kumsalimia tangu utimue kibati?[emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…