Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Mimi niliamua kuchomoka home sababu tu ya kuvaliana nguo na Bro wangu
Unapiga usafi wa nguvu chumban kwetu,, unafua mashuka, nguo zangu zinakua safiii,, ila Sasa br wangu yeye anajua kuvaa tu,, akishazishazichafua ajui kuzifua na kuziweka safi kama alivyozikuta,, anavaa nguo yako ata km umetoka kununua na bado mwenyewe ujaivaa,, yeye anaivaa ikichafuka anaitupa kule,, mpk uje mwenyewe kuisafisha nguo yako, ikiwa safi ataimendea ataivaa tena na tena ila kufua ndio mtihan, ila Sasa ukivaa nguo zake ugomvi mkubwa nikaona sio kesi nikaanza kujichanga kidogo kidogo nikipata vihela vyangu vya ufundi ujenz na vibarua vya hapa na pale nikatengenesha kitanda kikali cha mchanganyiko wa chuma na nakshi za mbao,, godoro langu la nchi 8..mashuka yangu kadhaa hata km msela sio unamiliki mashuka mawili ni uchafu unatakiwa ubadilishe hali ya kitanda kwa kutandika mashuka masafi mara kwa mara,, hata ukiingiza demu anaona kweli unajipenda mda wote akija anakuta kitanda kisafi mpk anakiogopa ,,, feni yangu ya dolphin ya nchi 19,, nikavuta subwoofer,, flat yangu nch 32 LG led tv na TV show case,, kisimbuz changu(Azam decoder ),,nikatengenezesha kistand changu cha chuma cha kishkaji ambacho kinahifadhi nguo juu na kati chin kina kishelfu cha viatu... Nikachomoka home na kupanga zangu getho mbali na home ili nipambane mwenyewe iwe hata ngumu kwenda kugongea menu (msosi)home... Ukilala njaa ndio Akili inakuja,,
NOTE ;Ambao ndio mnajipanga kuchomoka home ni vema ukajipanga kwa vitu muhimu maana ukishaingia keto kwa sis masela tunakabiliwa na Hela ya kodi, umeme, maji, takaka, vifaa vya usafi wa nyumba na choo na kujilisha mwenyewe pamoja na hela
Za kuhonga za hapa na pale hivyo ukipata hela yako kutoka kweny harakati zako za hapa na pale ndio utumika hivyo... Utajikuta unachukua muda mrefu kuongeza vitu muhimu kweny getho,, hivyo ukijipanga mapema inakua umejipa unafuu mkubwa....
WANA PANGENI MAGETHO YENU MUSIONE YA KWETU YANAPENDEZA NA KUNUKIA BASI NINYI NIKUAZIMA NA KUPIGIA SHOO TU,ALAFU MASHUKA MULIOLOWESHA TUFUE SISI WENYE FUNGUO ZETU... TUME ENYEKA MUJUE KUYAPATA...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom