Ulianzaje kukaa gheto?

Ulianzaje kukaa gheto?

Pole mkuu life ndo huwa hivyo

Mm kama mm sipendag maden nilipata changamoto kama yako kipind nimemaliz chuo hakuna boom wala nn ilipidi nianze kuchoma baadh ya vitu ilinipate kodi huku nikiendelea kupigana kuchoma vitu namaanisha kuuza baadh ya vitu nakumbuka niliuzaga fridge yangu ili nipate laki 3 ya kodi ila mwish wa siku kila kitu kilijiweka sawa kweny maisha utakuwa na aman kama unasehem yako ya kukaa kula inakuja baadae mm nilikula wali chai mpaka nikawa nikipakua msosi napata kichefchef ila maisha yakaenda
mwenzenu nlikua gheto, biashara yangu ikabuma....nkakosa pesa ya kodi ...leo hii tarehe 14.06.2019 nmepiga kitu inaitwa U-turn

haya maisha sjui sie wengine tumeyakosea nn
 
Pole mkuu Mungu atakujalia rehema zake utasimama tena, amini wewe sio wakwanza kudondoka mimi nilichoma laki 750 kwenye kuku na juice mkuu hiyo nilidunduliza tmiaka 3 ya chuo na biashara yangu ya kwanza ndo ikala mweleka...

ulikuw unafanya biashara gani na upo mkoa gani mkuu??
dar bro....biashara ya usafirishaji
 
mwenzenu nlikua gheto, biashara yangu ikabuma....nkakosa pesa ya kodi ...leo hii tarehe 14.06.2019 nmepiga kitu inaitwa U-turn

haya maisha sjui sie wengine tumeyakosea nn
Usife moyo mkuu hauko mwenyewe amini. Endelea kukomaa kikubwa ujue umetelezea wapi. Kwa watoto wa kiume hiyo kawaida kabisa, piga moyo konde.
 
Miminilimaliza chuo baada ya mwaka nikapata bonge la dili ndani ya mieizi mitatu nikapanga apartment Kunduch, nikanunua alteza, na fenicha zote za ndani na mazga zaga yote. Aisee kusema kweli nilianza ishi bila shida maana nilihamia nina kila kitu kuanzia kitanda, washing machine, friji na matakataka yote. But the good times hazi ku last for ever, baada ya miaka mitatu mambo yalinienda kombo balaa.
Malizia story mzee. What happened?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kwa kipiindi hicho nilikuwa naingiza pesa nilikuwa napiga project flani nakula karibu miasaba kwa week au zaidi ukichanganya na ujana na sina wa kunitegemea basi nilikuwa nakula bata na kusafiri safiri maana kazi niiliyokuwa ninafanya ilikuwa inaniruhusu kuwa mahali kokote ili mradi kuna masaa flani kama tatu kwa siku niwe online. Sasa project ilikuja kukata baada ya huo muda sina biashara wala nini ila nilikuwa nimeanza jenga sehemu na ndo kwanza ninaanza... Nilipigika mwaka mzima sema mambo yakajaa kaa tena japo si kama awali.
Pole sana mkuu. Ila ndio maisha ya ujana yanavyokuwa sometimes. Ukishtuka too late. Ila this time bila shaka hurudii tena ule ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23]yan sikumbuk hata zilienda wap pamoja na earphone zangu nilikuwa peku kama mwiz ogopa unaulizwa kwann upo nje ...nikisema msela yupo na demu ndan ningechoma maana dem wa msela alikuwa form 3
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwa hiyo sendo zilipopotelea hujui mzee? Ila watu wana historia sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23]yan sikumbuk hata zilienda wap pamoja na earphone zangu nilikuwa peku kama mwiz ogopa unaulizwa kwann upo nje ...nikisema msela yupo na demu ndan ningechoma maana dem wa msela alikuwa form 3
Kweli mzee inabidi ufe kishujaa tu. Lakini mwamba huko ndani anakula vinono ilhali wewe umetaitiwa na wagambo unashirikiana nao ulinzi shirikishi. Haya maisha hayapo fair kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom