Nilikaa home Sana pasi na kuwa na ajira.
Bi mkubwa alirudi siku moja akanipaga namba ya simu akanambia mpigie huyu mtu anatafuta mwalimu wa somo la TEHAMA kwenye college yake.
Nikapiga jamaa akasema niende ofisini na CV.
Nikaenda ofisini akasema sasa chuo chake ndio kinaanza hivyo hapatokuwa na mshahara wa maana mpaka pale wanafunzi watakapo jaa.
Nikaona isiwe shida ngoja nikomae kibishi. Nikawa nasaidia kutafuta wanafunzi kupitia mtandaoni. College ikajaa wanafunzi. Tukaanza kulipwa posho kila mwisho wa wiki, 15, 20 & 30 elfu ndio zilikuwa posho zetu. Walimu tukaendelea kukomaa ingawa posho ikawa aitoshi.
Mkoa niliokuwa naishi ulikuwa na maisha nafuu sana. Nikaamua nitafute ghetto lisilo na umeme la buku 10 kwa mwezi, ili tu nikwepe mizengwe ya home. Basi posho ikasaidia kuniweka gheto. Ingawa apo gheto maisha yalikuwa magumu. Nilijua ipo siku itaeleweka.
Wanafunzi wakaanza kujaa pale college..tukaona huu ndio wakati wa kumwambia mkurugenzi awe anatupatia pesa ya maana. Mkurugenzi akaanza kuzingua na kutuzungusha. Walimu tukawa tunaanza kuingia pale shule saa 3 asubuh tunatoka saa 5. Hama ilisepa kabisa.
Tukakaa na mkuu wa shule (alikuwa jamaa tu kama sisi) kupiga mahesabu ya mapato ya college tukaona chuo kinatakiwa kuwa na milion 6 kitu ambacho ingewezekana kupewa hata kilo 1 kila mwezi kwa walimu 4.
Kupeleleza tukagundua alienda bank akakomba pesa yote kushiriana na co-director. Wao ndo walikuwa signatory.
Nikaona useng.. ngoja niache kazi. Baada ya siku 3 nikaskia wenzang nao wamesepa.
Maisha yakawa magumu, kodi ya gheto sina wala pesa ya kula sina. Ikafila hatua nikawa naenda home naiba mchele, mafuta, unga na vitunguu naleta gheto. Pesa ya kodi nilikuwa naipata kihuni sana. Huwezi amini niliweza kulipa kodi kwa kubeti beti 500 na mwisho wa siku napata 12,000/= (wastani).
Katika kipindi iko nilikuwa nabeba laptop yangu naenda kweny grocery ya manzi mmoja niliyekuwa nakulaga. Pale nilikuwa nikifanya applications za kazi, kwa kuwa gheto halikuwa halina Umeme.
Jitihada zote ziligonga mwamba. Nikawa sina cha kufanya. Nikawa natamani kufanya kazi ndogondogo kama za deiwaka. Ila nikawa naona aibu kwa sababu wahuni wa kitaa walikuwa wananiita Mwl.
Nikaanza tabia ya kukopa pesa. Kwa kuwa watu wengi walikuwa wananiamini basi haikuwa changamoto sana kupata pesa. Watu walijua wanamkopesa Mwl kumbe muhuni maisha yamenifyonza kamasi.
Pesa nyingi nilikuwa nabeti.
MUONEKANO WA GHETO LANGU
Kagodoro kadogo kanako fanana na yale ambayo wanabeba watoto wa form one waendao boarding.
Kajiko ka gesi/ndoo ndogo 3/
Vyombo kadhaa vya kupika/kulia.
Hivyo ndo vitu vya thamani.
Sijawahigi kuleta manzi gheto wala walimu wenzangu kutokana na muonekano wangu ulivyo tofauti na ninapolala.
LONG STORY SHORT
Baadaye sana yaani, baada ya msoto mkubwa wa mlo mmoja kwa siku. Nilikujaga kubahatisha kushinda milioni 4.3 kwenye betting.
Nikaona ndio wakati wa kuanzisha biashara. Nakumbuka sikuwahi kutumia hata sh 100 kurekebisha gheto zaidi ya kulipa kodi ya miezi 4 yaani 40,000/= tu. Kiasi chote nilikiweka kwenye biashara ya kiduka cha vinywaji mbalimbali.
Sikuwa na uzoefu wala historia ya biashara ila ile biashara ilikuwa ikikua na kunisaidia sana. Nilianza kurekebisha gheto baada ya miaka 2 baadaye.
Nikawa sasa ninaishi maisha ya wastani na kulala pahala penye hadhi.
Baadaye nikaitwaga kwenye usahili kwenye shirika ambalo wala sikuwa nakumbuka kama nimeApply kazi.
Baadaye nikapata hiyo kazi, na nikaja gundua kuwa niliwahi apply miaka 2 nyuma kwenye nafasi ambayo hata sikuwa nimeitwa kwenye usahili..ila CV yangu ilikuja kuonekana baada ya nafasi kutokea.
Nikaajiri kijana awe anakaa dukani, mm nikaanza kazi pale. Maisha yakawa poa. Nika hamia kwenye nyumba ambayo nalipa kodi 100,000/= kwa mwezi...kutoka kwenye nyumba ya 10,000/= kwa mwezi.
Kumbuka nilihama home mwaka 2013. Sasa
Mwezi uliopita nilipita kijiweni ambapo nilikuwaga nabet. Nikakuta wahuni wanaendelea kupambana. Nikawapa moyo kuwa ipo siku watatoboa, then nikasepa.
View attachment 1720144