Sio muda mwafaka mkuu, Kwanza jua unataka nini na kwa wakati gani, me pia nilianza kazi na mshahara kama wako
Na kipindi hicho nilikuwa natoka mbali sana ili kwenda kazini, kama ni mwenyeji wa Dar, Me nilikuwa naishi sehemu moja panaitwa Kisewe, kupita mbagala na unaingia Chamanzi, unatokea Mbande
ilikuwa inanilazimu kuamka sa 10:30 usiku kujiandaa na hadi sa 11:15 napanda daladala kwenda kariakoo, nilikuwa nafika mjini sa 12:30-12:45 na kuondoka sa 12:45 jioni na home kufika sa 4 usiku
Pamoja na kupata kazi ila sikuona kama ni muda sahihi wa kuondoka home, ilibidi nianze kwenda kuwekeza hela kwa muuza godoro, nilianza kuwekeza 70k ili ninunue godoro Dodoma QFL inch 10 ambalo Kwa kipindi hicho lilikuwa likiuzwa 220k
Kutokana na nauli kuwa ndani ya hiyo hiyo pesa ndomana nikaw naweka 70k na kiasi kingine nilikuwa nahemea vyakula pale home, baada ya miezi 3 nikawa nimemaliza kulipia godoro na mshahara wa mwezi wa 4 ndo nikaenda kutafuta chumba Kigogo
Nilianza na chumba cha 30k nikalipia miez 3 na kununua baadhi ya mahitaji, ndipo nikahama home na kwenda kujitegemea rasmi, kwahiyo kama home hakuna ugai gai we kaza tu ata miez 3 ili ujiandae kisha usepe
Baada ya hapo ndo nikaanza kuweka tena hela ya kununua kitanda na baadhi ya vitu mdogo mdogo huku nikiendelea kulalia maandazi na marage ya kuomba hati punguzo ili nipate Kwa nusu bei
At least saizi Mambo sio mabaya sana maana naishi kwenye kanyumba kenye unafuu wa muonekano na ata ndani sio haba sana, mtu akija home hawezi kujua kama nilikuwa sina ata 200 ya kulipia huduma ya Choo pale kariakoo
Ukisema uondoke na hiyo 150k utaambulia chumba tu na kagodoro Ka hovyo alafu itakulazimu kuja kununua tena godoro lingine zuri kwahiyo utakuwa umeongeza gharama ambazo sio za ulazima na usiombe hicho kibarua kikaota nyasi mwezi wa 2 tu alafu uwe umesepa home mapema
Kama hapo ulipo sasa kero zilizopo au shida zilizopo zinavumilika basi we jipe Malengo na uishi malengo yako ili baada ya Muda uliojiwekea uwe umetimiza na kuendelea na mambo mengine ambayo
View attachment 2469212