Ulianzaje kusoma vitabu?

Ulianzaje kusoma vitabu?

nilianza kusoma vitabu baada ya kuhamishiwa english medium kutoka shule za serikali. kule nkakuta jamaa wanaongea ngeli hatari, shule ilikuwa na kila kitu. jamaa nkawa nagoma kwenda shule kwasababu sijui ngeli, mzee akaniuliza kama shule ina maktaba, nkamwambia ndio, akasema nianze kwenda/kuingia huko na kuangalia hata picha tu kwenye vitabu, nkaanza kufuata ushauri wake. baada ya muda, nikawa kila nafasi nliyopata naitumia kwenda library, nkajenga urafiki mzuri sana na librarian pia, maana sio wengi waliokuwa wanaenda library. kutoka hapo nkawa nimejenga mapenzi ya dhati na vitabu, na vitabu vya mwanzoni kabsa ni READER'S DIGEST ambavyo vilikuwa vinahusu dinasours
 
Habari zenu wakuu,

Kama ilivyo kwa wa Tanzania wengine swala la kusoma vitabu ni gumu sana kwetu hasa vijana na mara nyingi wazee ndo wamekuwa na utaratibu huo.

Leo nataka ku share na nyinyi my love story iliyonipelekea kuanza kusoma vitabu.

Nilikuwa kwenye mahusiano na binti mmoja niliyefahamiana nae kipindi nipo chuo Ila Mimi nilimtangulia mwaka mmoja mbele alikuwa darasa la nyuma yangu

Nilimpenda na yeye alinipenda pia na tulishirikiana kwenye shida na matatizo kwa nyakati tofauti pindi mmoja wetu anapohitaji msaada wa haraka.

Nilifanikiwa kumaliza chuo huku yeye nikimuacha bado akiendelea kwani tulipishana mwaka mmoja Kama nilivyoelezea hapo awali,
Sasa balaa ndo lilianzia hapo baada ya kumaliza maana bado tulikuwa tuna mawasiliano mazuri tu na tulikuwa tumefika level ya kushirikishana hata Mambo yanayohusu familia zetu na kushauriana baadhi ya Mambo mbali mbali.

Mambo hayakuwa mazuri kiupande wangu baada ya kumaliza chuo kwani changamoto ya ajira ni janga la taifa kwa Sasa , Basi tukawa tunaendelea kuwasiliana na Yule mwanamke Ila alianza kubadilika ghafla Tena kwa mda mfupi sana ikawa nikiongea naye nikimuuliza kitu ana nijibu anachotaka hata kuonana kukawa kwa masharti magumu Sana ikafika mda mpaka ananiambia we utanisaidia Nini katika maisha yangu Bora kila mtu afanye mambo yake tu .

Basi kwa kuwa tulipendana sana na mabadiliko yalikuwa kwa mda mfupi ikabidi nitafute sababu zilizo mfanya abadilike vile, Basi baada ya uchunguzi wa mda mrefu nikaja kugundua jamaa mmoja wa TRA ndo anakula mzigo na ana mhudumia kwa kila kitu maana huyo jamaa alikuwa ame-post wako pamoja beach katika pozi za kimahaba aisee niliumia Sana kwa kweli kwani Yule jamaa ilikuwa anagharamia kweli kweli na mara ya mwisho huyo demu alifanya field hapo TRA nadhani ndo walikutana hapo.

Stress za kutoswa na msoto wa ajira na kupigiwa na jua Kali nikaangukia kwenye usomaji wa vitabu ili kupunguza machungu japo kidogo, na kitabu changu Cha Kwanza kusoma kilikuwa kinaitwa "UNDERSTAND THE PURPOSE AND POWER OF MEN" by Dr Myles Munroe baadae nikawa nasoma vitabu mbalimbali kama THINK AND GROW RICH-RICH DAD POOR DAD -HOW TO WIN FRIEND'S AND INFLUENCE PEOPLE na vingine vingi na mpaka sasa bado naendelea na utaratibu huo kwa Sasa nasoma "THE 100 START UP" but now I'm good mungu anasaidia kidogo si haba na tunaendelea kupambana na life japo ilinichukua mda kidogo kukaa sawa.

Wewe je ulianzaje zoezi hili gumu kwa watanzania wengi ? Karibuni wadau tujifunze wote .
Nilivoona jina la kitabu tuu POWER OF PUSSY fastaa nikatamani kujua yaliyomo ndo nikawa msomaji mzur now nasoma THINK LIKE A MAN ACT LIKE A LADY.
 
Kila kitabu nachopitia kwa kweli kwangu huwa ni favourite. Kwa sababu kila kimoja uwa na madini yake unique kabisa.

Ila na-recommend

1. How to win friends and influence people.
2. The Airbnb Story
3. Dark Psychology
4. Zero to One
5. 10X Rule
6. Men are from mars and women are from venus
7. Falling Forward
Ase ni vingi sana, natamani watu wasome
VINGI MNO.
Men are from mars, ni kizuri mno kwa mtu interested na issue za mahusiano, pia THE POWER OF PUSSY wnawake kisomen hiki
 
Back
Top Bottom