Ulianzaje kuvuta bangi?

Mbwa dume

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
5,934
Reaction score
10,206
Mie nilianza rasmi kuvuta bange miaka ya 2001.

Iko hivi:
Baada ya kufeli darasa la saba mwaka 1998 (sababu sikuwa na akili darasani) kipindi hicho mzee akamind sana ikabidi nisepe zangu mikoani kusaka mishe.

Nimepiga zangu mishe mishe za town miaka kadhaa ndo nikakutana na jamaa mmoja alijulikana kwa jina la Dura. Alikuwaga mpigaji flani wa hizi mishe mishe za mjini ikiwemo wizi wa mafuta ya transformers na vyuma chakavu.

Huyo jamaa ndo alinishawishi nikajiunga na group lao tukaanza rasmi wizi wa mafuta ya transformers ambayo kwa kipindi hicho yalikuwa yanalipa sana na tulipata hela sana kipindi hicho, japo kazi ilikuwaga ngumu na ya hatari sana kiasi kwamba nilijikuta naanza kuvuta bangi na hao masela wangu.

Bange ilituongezea ujasiri na umakini kwenye mission zetu zote na kiasi flani tulifanikiwa kupata hela na kuanza kumiliki mageto ya maana (japo tulikuwa tumepanga).

Ila ndo hivyo hakuna marefu yasiyo na ncha, miaka kadhaa mbele likatokea tukio baya tukiwa kwenye transformer flani; kuna makosa yakatokea ikaripuka wenzetu watatu walikufa hapo hapo na tuliopona tulijeruhiwa vibaya sana kiasi kwamba ilichukua muda kuwa sawa na ndo ikawa mwisho wangu wa hizo mishe.

Ingawaje sasa nishakuwa mtu mzima ,ninamiliki biashara kubwa ya majeneza ndani na nje ya mkoa lakini huwa navuta bange mara moja moja japo kwa siri sana, maana mwonekano wangu haufanani kabisa (ni bonge la mtu kiasi kwamba wasiofahamu biashara yangu huwa wanajua ni boss flani kwenye kampuni) [emoji1787].

Je, wewe ulianzaje kuvuta huu mmea?
 
Uliamua kuanza kuuza majeneza ili kuwaenzi wenzako waliotangulia au uliona ni kazi unaoimudu?
 
Uliamua kuanza kuuza majeneza ili kuwaenzi wenzako waliotangulia au uliona ni kazi unaoimudu?
Ni story ndefu kidogo nitaelezea siku ingine ila kifupi naipenda sana hii biashara maana kwa kiasi flani imesaidia sana kubadiri maisha yangu!
Nimeweza kujenga, kusomesha watoto na pia nimenunua kagari(kama kale ka mr Bean)
 
Nimeshairipoti hii thread, itafutwa punde
 
Nikiwa kidato cha tatu Chemistry imenikolea teacher wa Physics kanitangazia vita. Home mshua wangu kafariki na brother angu kipigwa risasi kweny lile tukio kibiti karo ya shule imekua yakuchanga.
Aiseh acheni
 
Nikiwa kidato cha tatu Chemistry imenikolea teacher wa Physics kanitangazia vita. Home mshua wangu kafariki na brother angu akipigwa risasi kweny lile tukio la kibiti karo ya shule imekua yakuchanga.
Aiseh acheni
Umeacha?
 
[emoji23][emoji23] hii ndo jamii forum
 
Bado sijaacha hapo natumia mara chache sana
Ni kweli kwamba marijuana inabagua watu. Kuna mwingine inaweza kumfanya kichaa? Maana natamani sana kuja kutumia ila hofu yangu ni kuwa pengine ikanikataa nikawa kichaa au kufanya mambo ya ajabu mtaani. Ninawaza sana. Ila kweli toka moyoni naipenda sana marijuana.
 
Nyonga Choma Vuta zungusha kijiti piga pafu wapasie wengine,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…