Ushimen
JF-Expert Member
- Oct 24, 2012
- 40,828
- 99,523
Sio poa kabisa mwamba, hata kama unamiliki chuma ila dahh ulizingua kinyama.
Ipo hivi.... Mnyama nilijilipua kiwanja flani last night, mara kwa mbali wakati natoka nje nikaongee na sim nikawa nimepishana na klaree, ndo vile sikumchelewesha kwa swaga.
Sasa nilipo maliza kuongea ma sim, kwambaaali nikamuona du anaelekea upande wangu, sasa kwakuwa pembeni palikuwa na cars parking nami nikajisogeza na nikachagua chuma kidogo yenye hadhi (BMW-X5) nikaiegamia kwa mikogo kama yote.
Basi mtoto alipo sogea nikameamesha na nikaanza kumwaga sera huku mkononi nikitikisa ufunguo wa sanduku (unaki holder cha maana) wenye kufanana na funguo ya gari, basi mara klaree ajichekeshe mara ajibebishe ilimradi fuli mbwembwe tupu.
Sasa kumbe kwenye ile chuma palikuwa na jamaa, mara akaiwasha ili BMW na akaanza kurudi nyuma (reverse) huku akiniacha na aibu na bidada akaondoka na kuniona kapuku huku akiachia msonyo mrefu.....
Yani kwa hasira nikamsogelea mwamba pale alipo sogea na chuma yake na nikamuona anaperuzi jf, ila nikaamua kukausha nikasema lazima nije nimchane aiseeee.
Sio poa kabisa mnavyo tufanyia wakuu mnao miliki magari.
Yaani jamaa aliniharibia siku, nikaamua niondoke hata maeneo yale nikaenda kujilipua na K-Vant kubwa kuleee uswahilini kwetu.
Hapa ndio kwanza naamka yani Dah...!!
Sent using Jamii Forums mobile app