Ulichukuwa hatua gani ulipotambua unachukiwa bila sababu au unaonekana huna msaada wowote kwa waliokuzuguka?

Ulichukuwa hatua gani ulipotambua unachukiwa bila sababu au unaonekana huna msaada wowote kwa waliokuzuguka?

Mia saba

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
255
Reaction score
390
Hiko hivi,

Nimepata masimulizi kutoka kwa jamaa yangu sana yanayomsibu.

1. Ni mtu wa moyo Safi, Ila atawale aliowasaidia wanamuona nonsense kwa sasa

2. Anasema wakati fulani anasaidia kutoa taarifa kwa marafiki chimbo wanapopata mzigo kea Bei rahisi Ila jamaa zake wakipata sehemu nafuu zaidi wanakaa kimya

3. Kwenye mazungumzo akianza kuchangia mada watu wanahairisha story na kuendelea na shughuli zako

4. Anapambana more lonely sana bila campany vikampelekea:

1. Mawazo Sana

2. Pombe Sana

3. Nyuchi kidogo

Madhara aliyopata

1. Baadhi ya biashara kaanza kufunga

2. Mauzo kichache mno

Ushauri wangu

1. Asiache kusali

2. Kila Jambo linakuja na maana yake hivyo pamba Usikate tamaa

Je hii hali ni kawaida kweli?
 
Mimi nimechukiwa na mdada mmoja hapa jirani yangu hadi nimeshangaa aisee, yaani bila sababu nilikuwa nawasiliana nae kawaida tu ghafla nikimsalimia anakunja akafuta na namba yangu kila kitu yaani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nimechukiwa na mdada mmoja hapa jirani yangu hadi nimeshangaa aisee....yaani bila sababu nilikuwa nawasiliana nae kawaida tu ghafla nikimsalimia anakunja...akafuta na namba yangu kila kitu yaani....[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Umechukua hatua gani kukabiliana na hiyo Hali maana sumu husambaa taratibu
 
Hao wanaomchukia kuna namna wanamfanya akose kipato au mademu? Kama jibu sio mwambie aache kujipa umuhimu kwenye maisha ya wengine. Aishi maisha yake. Ukute anaona tu wenzie wanamchukia sababu anajishtukia.
 
Leave them alone mind ya own bizness, jifanye huwajui, tafta pesa uwe above them yaan tukio likitokea tu toa hela kuwazidi wao hala kaza msimamo wako wakutotaka chawa,, yaani hiyo kitu itaturnback kwao wao ndo wataanz kuumia balaa
 
Siku moja nilimtembelea rafiki yangu aliye kipofu. Kwa sababu ilikuwa usiku alifanya kitu kilichonifundisha sana. Nilipoingia ndani, Moses aliwasha taa. Nikamuuliza, Moses, kwa nini umewasha taa wakati wewe huoni? Moses alicheka sana, akazima taa na kuelekea jikoni, kitambo kidogo akaja na chupa ya chai na mayai, akaviweka mezani kwa usahihi kabisa na akawasha tena taa.

Moses alichokisema kilinitoa machozi aliponiambia, Daudi! Sikuwasha taa kwa ajili yangu au kwa uhitaji wangu, ila kwa ajili yako wewe unayeona kwani wewe siyo kipofu kama mimi. Halafu akaniuliza, "Daudi!! Ni mara ngapi umewazimia taa wengine ukiwanyima fursa ya kuona mwanga kisa tu wewe huuitaji? Nilifikiri juu ya hilo kwa kina. Nami nakuuliza swali hilo leo, Ni mara ngapi umezima taa na kuwanyima wengine fursa ya kuona mwanga walipokuwa gizani?

[emoji2369] Kwanini akaunti yako iwe na mamilioni huku mtoto wa ndugu yako akitembea bila viatu? [emoji2369] Kwanini unatupa nguo usizovaa jaani wakati kuna anayekaribia kutembea uchi? [emoji2369] Kwanini vyakula vinaoza nyumbani kwako wakati kuna anayelala njaa?

[emoji2369] Kwanini unaona fursa ya biashara na kuificha bila kuwashirikisha rafiki zako kisa wewe huihitaji? [emoji2369] Kwanini uko na nafasi ya kumsaidia mtu kupanda cheo au kupata ajira mpya hufanyi hivyo kwa sababu wahusika sii wa kabila lako au dini yako?

[emoji2369] Kwanini unawachafua ndugu zako sababu hutaki mwingine awasaidie? Kila Swali Hapo Juu ni Sawa na KUZIMA TAA!! Haya tuyaweke akilini kama Wanadamu. Tuanze kulenga yanayompendeza Muumba wetu na Ubinadamu. Hii ndiyo dini ya kweli, kuwasaidia wahitaji, wasiojiweza na wasiosikilizwa. TAFADHALI WASHA TAA ULIZOZIMA! "Wewe ni nuru ya TAIFA LA MUNGU."
 
Ni kumuomba tu Mungu na kuishi kivyake vyake hamna haja ya kusumbuana na watu, kuishi na watu ni kazi sana.
 
Thanks
 
Hiyo ni kawaida sana wenye neema flani flani....kuchukiwa bila sababu na hata kutengwa..huwa wanahisi wakifanya hivyo watakushusha au kukuumiza...kama unajitambua wewe fanya yako.....
 
Kata misaada ya kipuuzi

Jenga maisha yako

Miaka hii bado mtu unahabgaika na marafiki na jamaa kwani alizaliwa nao?

Si alikuwa peke yake tumboni kwa mama yake????
 
Wamesha chezea himaya ya kiroho ajiwahi haraka kabla hajaanza kusafisha jiji maana ana dalili zote za kutupiwa karma.
 
Binaadamu wameumbiwa wivu,usio na mbele Wala nyuma.Jamaa apambane kivyake Tena kimya kimya
 
Back
Top Bottom