Ulijiepusha Vipi na Urafiki Mbaya? Niliponzwa na Urafiki na Wabaya

baba bora

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2016
Posts
1,500
Reaction score
1,093
Wazazi wangu walikuwa wakinikataza kushirikiana, kucheza na baadhi ya watoto wenzangu
Sikuwa msikilizaji nzuri wakati huo. Nilijiambia hawa Ndio marafiki zangu

Nikiwa darasa la Saba rafiki yangu kipenzi alidokoa dukani kwao kiasi cha 30000 Alitumia pekee yake. Mzee wake alipogundua alimcharaza viboko hatari
Rafiki yangu kipenzi akanitaja kuwa Mimi Ndio nilimsonga kuiba

Msala ukahamia kwangu nilikula kichapo kwa mzee hadi kushusha haja ndogo toka hapo Urafiki ulikufa

2009 Nikiwa secondary rafiki tulieambatana Kama ndugu muda Wa darasani, kula, michezo na bwenini tulikuwa wote tulikuwa hatupo wote muda mchache Sana hasa Usiku

Jamaa yangu alikuwa mlevi ana vuta bangi pia yani baada ya prepo kuisha anaruka fensi anazama machimbo yake kitaa
Siku ya jumapili ya mwisho Wa mwezi Wa nne aliniazima begi langu la daftari aende nalo chimbo

Akasahau kutoa Kete 2 Za bangi na viroba kwenye begi jumatatu kunadada aliibiwa wakaja walimu kusachi nilikutwa na bangi na viroba nilifukuzwa shule Siku hiyo hiyo

Asubuhi nikapakizwa gari kurudi nyumbani mzee akanitimua naye hakutaka kusikia chochote toka kwangu
Niliishi kwa baba mdogo mzee alikataa Kabisa kunirudisha shule alikuwa anasema siwezi somesha mvuta bangi Mimi niliumia Sana
Mwezi Wa kumi 2009 mzee aliniita nyumbani nilifurahi Sana nikajua nimesamehewa narudi shule.

Haikuwa hivyo nilitafutiwa gereji ya magari niliumia Sana Urafiki Mbaya ulinigharimu Sana

Wewe ushaponzwa na Urafiki ? Ilikuwaje?
 
Natamani kujua mwisho wa stori yako. Je mpk sasa ni fundi garage au..?? Au dingi alikurudisha shule tena...!!!??
 
Inategemeana mbona mimi ni mvuta bangi,mnywa pombe aina zote,mtafuna nyasi,mla madem.Lakini sijawahi fukuzwa shule wala kufeli.

Mimi ndio rafik mbaya mwenyewe sijajiharibia how come rafik aniharibie.
 
Inategemeana mbona mimi ni mvuta bangi,mnywa pombe aina zote,mtafuna nyasi,mla madem.Lakini sijawahi fukuzwa shule wala kufeli.

Mimi ndio rafik mbaya mwenyewe sijajiharibia how come rafik aniharibie.
Daaah mkuu we ni hatari... Nijuavyo bangi na mademu mbali sana
 
Tatizo lako,ulikuwa zoba alfu una marafiki wajanja!ulitakiwa uwe na zoba wenzio!miye nlikuwa mjanja na friends pia!kila mtu anakufa na tai yake shingoni!
 
Marafiki yangu wengi niliokuwa nao walikuwa watukutu sana yani ile mzazi hawezi kuruhusu kuwa na urafiki nao. ndio ilivyokuwa hivyo nashukuru sikuwahi kuwa na tabia kama zile japo ndio walikuwa friend zangu sana.

Umenikumbusha msala mmoja walifanya washikaji zangu kiskuli skuli kulikuwa na walimu wa zamu wanazingua sana time ile sasa mida ya prepo night washikaji wakajipanga kuwaletea zengwe usiku ule washikaji waliwazingua sana wale waalimu kwa kuwapiga viboko na mawe.
Sasa kutokana ndio nilikuwa marafiki zangu baada ya shule nzima kupigishwa kwata ikabidi watajwe na kundi zima nikiwemo japo ndio vile kosa si langu ila marafiki tu.

Kesi ilikuwa kubwa sana ya kupiga waalimu. Tulikaribia kufukuzwa shule na yule dogo aliyenitaja hadi kesho siwezi kumsahau.
 
Tatizo lako,ulikuwa zoba alfu una marafiki wajanja!ulitakiwa uwe na zoba wenzio!miye nlikuwa mjanja na friends pia!kila mtu anakufa na tai yake shingoni!
Mkuu mtu kasahau dawa na viroba kwenye begi lako hujaviona unazama nalo class... Walimu wanavikuta.. Sikupewa nafasi ya kujitetea Muda huo huo nilifungiwa ofisi ya mlinzi Asubuhi nilisafirishwa home... We ungetokaje kwenye huu Msala
 
Uvuti Dawa Sawasawa utakuwa..... Lakini ujawai pata Msala sababu ya Urafiki na mtu
Kuna mchiz wangu wa damu tulisshawahi kuingizana kwenye misala wote.Mara ya kwanza yeye ndo aliniingiza kwenye msala nikapewa adhabu ya kupasua kuni mita mbili shuleni boding.

Uliofuata mimi ndo nlimuingiza kwenye msala akala suspension wiki tatu plus kuja na mzazi.

Misala yote ilihusu madem.

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Urafiki Mbaya una gharimu Sana... Kichwa kichafu
 
Haha Jamaa akumind... Mm Jamaa aliefanya nikafukuzwa shule sijakutana naye tena
 
Una tatizo la kuchagua aina ya marafiki na kuwaamini watu mapema (usiporekebisha hili litakugharimu sana maishani). Kwa mfano mtu wa aina yako (kama unavyodai ulikuwa) unaanza vipi kuwa na rafiki mliyetofautiana naye tabia kwa extent hiyo? (Rafikiyo wa viroba na ganja). Ukitumia criteria hizo unazotumia kutafuta marafiki kwa kutafuta MKE hakika utajuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…