Ulijifunza nini katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014/2019? Unatarajia nini katika uchaguzi wa 2024?

Ulijifunza nini katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2014/2019? Unatarajia nini katika uchaguzi wa 2024?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Tanzania inatarajia kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024, je, utashiriki katika Kupiga Kura?

Kama ndiyo/hapana kwanini?

JamiiForums inakukaribisha kushiriki katika Mjadala utakaohusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, utakaofanyika kupitia XSpaces, leo Agosti 22, 2024 Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku ukiangazia kilichotokea kwenye Chaguzi za 2014 na 2019 na hali iliyopo sasa.

lge.jpg

Kushiriki mjadala kupitia XSpaces ya JamiiForums bofya hapa

UPDATES:

JAFARI S. MNEKE, MKURUGENZI WA MAMBO YA NJE, SERA NA BUNGE - CUF

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Msingi wa Mamlaka, Utawala, Uwajibikaji na Maendeleo ya Nchi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Msingi muhimu wa Demokrasia unaowezesha Wananchi kuchagua Mamlaka itakayowaongoza

Wote tunajua Mwaka 2019 tulipaswa kuwa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini sote tunajua kilichotokea

Ule haukuwa uchaguzi bali Uchafuzi wa Demokrasia

Novemba 27, 2024 tunatarajia kuingia kwenye Uchaguzi wa Serikali za MitaaNinapata Matumaini kuwa wa Mwaka huu utakuwa ni uchaguzi tofauti na Uliopita ambao siuiti Uchaguzi bali Uchafuzi wa Demokrasia

Kwanza tumeona dhamira njema ya Rais wa Awamu ya 6 kupitia 4R zake

Pia, kuna ushirikishwaji, Wadau wa Demokrasia wakiwemo Viongozi wa Vyama vya Siasa, walishiriki katika Vikao ambapo tulitoa mapendekezo ya kuboresha Uchaguzi

DEDAN CHACHA WANGWE
Vijana tunatamani sana tuwe miongoni mwa wale watakaoshiriki katika Uchaguzi hata kwa mara ya kwanza

Mnakumbuka CHADEMA tulitoa msimamo wa kutoshiriki katika Uchaguzi huu hadi pale Katiba Mpya itakapopatikana lakini Vijana tunaweka presha ili Chama kishiriki

Ni rahisi kuwaongoza watu wenye njaa lakini ni ngumu zaidi kuwaongoza watu wenye njaa kali

Kwa jinsi hali ilivyo ni kama tunapoteza matumaini na chaguzi hizi ambapo sitamani tufike hapo kama Vijana

GWAMAKA MBUGHI
Nchi yetu tunachangamoto kubwa, kwamba Uongozi wa Serikalini ni lazima utokee kwenye Vyama vya Siasa

Kwamba mtu hawezi kugombea nafasi za uongozi kama hatokani na Chama, lazima adhaminiwe na Chama cha SiasaSasa mtu kama ana sifa lakini hayupo kwenye Chama cha Siasa, mfumo unawatupilia nje

Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tunapambana na Chama kimoja ambacho kimejigeuza 'Refferee' wa Uchaguzi

Mazingira kama haya yanavunja Watu moyo kushiriki katika Chaguzi za Serikali za Mitaa

Ndio maana kuna watu bado wanapambana kwamba Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi badala ya TAMISEMI

Tusiposhiriki Uchaguzi hatuwezi kutambua udhaifu wa Mifumo iliyopo. Tunapaswa kushiriki uchaguzi pamoja na changamoto zilizopo ili tujue matatizo na changamoto za chaguzi zetu

Tunapaswa kuendelea kudai Mifumo na Sheria bora lakini wakati huo huo bado tunashiriki Uchaguzi

GERVAS MAIKO
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaohusisha Vyama vingi vya Siasa tunajua haujawahi kuwa wa Haki kwasababu ya nani anayeendesha Uchaguzi

Hapo tulipo, hata baada ya kutengeneza wanachokiita Tume Huru ya Uchaguzi bado tatizo lipo palepale kwasababu Uchaguzi unasimamiwa na Mkurugenzi na TAMISEMI, ambao wote wapo kwenye Mfumo wa Chama cha Mapinduzi

Kanuni za Uchaguzi zinazotungwa na Waziri zina mapungufu makubwa na zinazokusudia kukipa Ushindi Chama cha Mapinduzi

Mazingira haya hayajabadilika kwa nia ovu, kwa maana hiyo tunapoenda ni giza neneNakubaliana na walioenda Mahakamani kupinga

Wakati wa Uchaguzi ni wakati pekee unapeleka Elimu ya Uraia kwa Wananchi Ukisusa ni furaha kwa Chama cha Mapinduzi. Na Sheria ya Uchaguzi inasema kama kuna mgombea mmoja anapita bila kupingwa

Kwahiyo sio vizuri kususa. Tushiriki tuwaeleze Wananchi ili wakihujumu, Wananchi watajua ni kwasababu ya Mazingira mabovu ya Uchaguzi

Wanaopuuza Uchaguzi ni wasomi, saa nyingine hata hawapigi kura lakini wajue kuwa Kiongozi atakayechaguliwa bado ni Kiongozi waoNdio pale tunabaki na usiposhiriki kuchagua Kiongozi utaongozwa na Kiongozi mjinga

Tunalaani dola kuwatisha Watu kushiriki Uchaguzi. Matukio ya kamatakamata yameanza, hii sio nzuri Watu wapo tayari kushiriki Uchaguzi lakini changamoto ni mfumo wa Dola, wameanza kuwatisha

THE GENERAL (MDAU)
Ni ngumu sana kushiriki katika uchaguzi kama hakuna misingi mizuri ya Uchaguzi, pia hakuna umoja wa Vyama, mfano uchaguzi huu kama wangekuwa na nia ya mabadiliko ya kweli wangeweza kuungana na hiyo ingeleta matumaini

NTEGHENJWA HOSEAH (TAMISEMI)
Kuna tofauti kati ya Daftari la Kupiga Kura na Daftari linalotumika kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mtaa

Uboreshaji unaoendelea hivi sasa Mikoa tofauti unakupa sifa za kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 lakini haukupi sifa za kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mtaa

Orodha ya Wapiga Kura kwaajili ya Serikali za Mtaa ni kuanzia Oktoba 2024, baada ya hapo ndio watakuwa wana sifa ya kupiga kura-Hivyo, inatakiwa Watu waelewe kuwa kuna madaftari mawili tofauti, kuna la Kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Mtaa

Tumefanya mchakato shirikishi kuelekea katika mchakato huu wa Chaguzi, kulikuwa na Wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi mbalimbali pamoja na Wananchi

Tumeshirikisha Mawazo na michango iliyotolewa na Wadau mbalimbali, hakuna haja ya kuwa na hofu, tumejipanga kuwa na Uchaguzi Huru na Haki, kama ambavyo tumeanza kwa Utulivu basi tumalize kwa Amani na Utulivu

JAFARI S. MNEKE, MKURUGENZI WA MAMBO YA NJE, SERA NA BUNGE: CUF
Ukilinganisha tulipotoka na tulipo, kuna dhamira njema inaoneshwa na Serikali iliyipo madarakani

Kama Rais wa sasa anakiri kuwa kulikuwa na changamoto huko nyuma na anaonesha dhamira njema, mimi ni nani nipinge?

Mimi sio mtu wa kuwaza ‘hasi’ napenda kuwa Mtu ninayefikiri ‘chanya’, kila zama zina kitabu chake, kila kiongozi ana zama zake

Demokrasia haizaliwi ikakua na kukomaa siku moja, lazima ipite katika mchakato, sitaki kuwa mtumwa wa Historia kuwa kilichotokea Mwaka 2019 basi kitatokea sasa hivi tena kisha nianze kukata tamaa

Nina imani kwa ushirikishwaji huu kupitia Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na katika vikao mbalimbali tunapata matumaini kuwa tunapokwenda kuna nafuu, sisemi kuwa Chaguzi zitakuwa na haki kwa asilimia 100 lakini naamini kutakuwa na nafuu kubwa

Tumeshawaambia Serikali mapungufu yaliyopo katika mchakato wa kuelekea katika Chaguzi zijazo na wameahidi kutekeleza hilo baada ya muda mfupi

Demokrasia ina uwanja mpana, hivyo inapotokea kuna Watu wanaenda Mahakamani ndio Demokrasia yenyewe hiyo

Sisi CUF tunataka Siasa za hoja sio Siasa za chuki, nchi yetu inaamana kubwa kuliko maslahi ya Mtu mmoja mmoja, CUF ni wahanga wa Siasa za chuki, hatutaki kurudi huko tulipotoka

WAKILI WILLIAM MADUHU (LHRC)
Mwaka 1972, Mwalimu Nyerere alifuta Mamlaka za Serikali za Mtaa zote kwa maelezo kuwa hazikutimiza majukumu yao sawa sawa. Mwaka 1976 kukaibuka Kipindupindu ambapo baadhi ya Mamlaka zikarejeshwa

Mamlaka hizo zilirejeshwa Mwaka 1982, huko ndipo tulipotoka, lakini tulipo sasa Viongozi wengi wa Serikali za Mitaa hawana mishahara na hawana posho nyingine tofauti na ilivyo kwa Wabunge

Mbali na hapo Viongozi wa Serikali za Mitaa wamekuwa wakiingiliwa katika majukumu yao, mfano inaweza kutokea Mkuu wa Mkoa au Waziri anamuondoa kwenye nafasi yake Kiongozi wa Serikali za Mtaa, mamlaka ambayo hayapo kwake kwa kuwa Wananchi ndio waliomuweka madarakani

Kwa ufupi Serikali za Mitaa zinachukuliwa poa licha ya kuwa zina umuhimu mkubwa wa kuendesha Jamii na Wananchi kwa jumla, hili jambo sio sawa

Viongozi wa Mtaa hawana maslahi mazuri, hawana ofisi na wengine mazingira yao ya kufanya kazi sio mzuri
 
Tanzania inatarajia kufanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 2024, je, utashiriki katika Kupiga Kura?

Kama ndiyo/hapana kwanini?

JamiiForums inakukaribisha kushiriki katika Mjadala utakaohusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, utakaofanyika kupitia XSpaces, leo Agosti 22, 2024 Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku ukiangazia kilichotokea kwenye Chaguzi za 2014 na 2019 na hali iliyopo sasa.


Kushiriki mjadala kupitia XSpaces ya JamiiForums bofya hapa x.com
CCM ni wakatili sana
 
Nilikata tamaa mara kadhaa lakini nadhani wakati huu itabidi nitumie nguvu yangu ya kidemokrasia kukatisha maisha ya kisiasa ya baadhi ya watu ninaowawaza.
 
Natarajia ccm itashinda kwa kishindo nadhani inaweza kuwa kwa 200%.

Msimamizi wa uchaguzi ni tamisemi na waziri wake kashasema hakuna nafasi hata Moja itaenda upinzani, wasimamizi vituoni watakuwa ndugu zetu watumishi wa tamisemi.

Vyama vya upinzani wangefanya mambo mengine wakaacha na uchafuzi WA aina ambao wanatumia rasilimali kwa kitu ambacho hakipo.
 
Ule ulikuwa ni uchafuzi na si uchaguzi.
 
Huu uchaguzi huwa unaacha chuki mitaani/vijijini maana nyote mnajuana kiukoo na familia

USSR
 
Back
Top Bottom