Ulikabiliana vipi na changamoto za uchawi?

Ulikabiliana vipi na changamoto za uchawi?

fatherhood

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2021
Posts
537
Reaction score
556
Habari JF.

Kwenye jamii zetu kuna changamoto nyingi sana ikiwemo uchawi . Kama vitabu Vingi vitakatifu vinavyosema uchawi upo.

Direct kwenye mada nakumbuka way back nipo form 3 , huku kijijini kwetu nilikuwa naumwa sana kiasi ambacho nilikuwa siwezi kusoma kabisa.

Hali hii iliendelea kwa muda kama miezi mitatu nilikuwa nasumbuliwa na kichwa na mgongo hali ambayo sana sana ilikuwa inanitokea nikiwa mazingira ya shule nikirudi nyumban mzima kabisa.

Hii hali ilipelekea kusinzia na kulala darasani ilikuwa haipiti wiki bila kwenda hospital , nakumbuka tulizunguka hospital nyingi sana ila hali ilikuwa bado.

Wazazi ni watu wa dini sana hawaamini katika ushirikina ilikuwa ngumu kuhisi kama mambo ya kiswahili yamehusika , basi afya ilizorota huku uwezo wa darasani ukishuka kutokana na kusumbulia sana.

Kama ujuavyo karibia kila familia kuna ndugu mmoja huwa anapenda mambo ya kishirika ila sio constant , basi ilikuwa kama masihara dingi mdogo alikuwa tofauti na wazazi wangu kwani yeye alikua anaamin kabisa mim nimelogwa.

Basi baba mdogo akanipeleka kwa mganga fulani maaneo ya huko kwetu lakin kwa sasa amehama kule kijiji ,basi yule mganga alinisaidia mpaka leo sisumbuliwi na kitu chochote .

Nimefungua uzi ili kushare experience ulikabiriana vipi au unaendelea kukabiriana vipi na changamoto za uchawi kwako wewe ama familia yako
 
Bila kujali dini zetu tujifunze kuisoma Ayatul kursi, Inafukuza kila aina ya machawi. Nimeona kitu cha ajabu sana leo kumbe kuna GUN DRONE CAMERA...
 
Ulilogwa au ulikua unalalia godoro lililoisha mgogongo unakutana na chaga
 
Natafuta nyumba ambayo watu wanaamini ina mashetani au vibwengo au vinyamkera au zindiko au mizimu au mauzauza nihamie. Mimi siamini kabisa kuwa kuna nyumba za namna hiyo na naamini ni imani au woga wa watu tu. Anayejua ilipo nyumba kama hiyo anajulishe ili tuweza kufanya mpango nihamie.
 
Ulikuwa na matatizo ya kisaikolojia tu mganga akafanikiwa kukuweka sawa. Imani huumba.
 
Walozi wanafanya kazi za ibilisi na wameshajihakikishia nafasi kwenye ufalme wa kuzimu, ni swala la muda tu....
 
Maombi na tiba asili vyotw vinafanya kazi , tatizo wengi wabajumuisha tiba asili na uchawi kitu ambacho sicho, leo hii nyumbani kwangu washenzi wakianza kuja usiku wanaweza kupakimbia endapo nafanya maombi ama nikichoma ule mmea ambao huwa unafukuza mbu, ni kitu kile kile tu isipokua maombi yanahitaji uwe mcha Mungu sana usiwe mtu wa dhambi dhambi.
 
Back
Top Bottom