Ulikabiliana vipi na ndugu waliokuzonga baada ya kupata ajira

Ulikabiliana vipi na ndugu waliokuzonga baada ya kupata ajira

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Wale wa kishua wanaweza wasinielewe sana. Ila wale wanaotoka familia za hali duni kama mimi mtanielewa.

Ukishapata ajira rasmi hasa serikali ndugu huja kama manyingu kutaka misaada. Hiyo inakuwa kabla hata hujajipanga vizuri bado unajitafuta. Sijui wewe ulikabiliana nao vipi.

Kwangu baada ya kupata ajira rasmi private sector hali ilikuwa inatisha. Nilijua nilikuwa na wajibu wa kusaidia ndugu na jamaa lakini sikutegemea kama itakuwa ghafla namna hii.

Bahati mbaya hakukuwa na mtu aliyenifunda namna ya kukabiliana nalo, nikachagua shortcut ya kubadilisha line ya simu tu. Nikabaki na wazazi, ndugu wa damu na ndugu wengine wachache ambao ni waelewa. Nilikata mawasiliano miaka kadhaa ili kujiweka sawa kwanza.

Kumbuka ndio kwanza nimetoka chuo, hata kitanda sina, lakini baba mdogo anataka umlipie mwanae ada anasoma private, baba mkubwa anafanya kilimo akaomba mtaji. Mwingine anasema tumekulea sasa zamu yako kulipa fadhila.

Wewe ulikabiliana vipi
 
Njia ni moja tu Privacy ,

unapata ajira unatangaza kwa ndugu,jamaa na marafiki unategemea wasikupige vizinga? badala ya kutulia mpaka pale hali itakapo kuwa shwari.

Siri ni muhimu kwenye kila jambo
 
Vicious circle ⭕️ of poverty… Waambie hapana… kama huwezi waambie umefukuzwa kazi
 
Mhimu ni kujifunza kuwa na roho ngumu tu, ukicheka na nyani utavuna mabua kumbuka siku ukifukuzwa kazi wao ndio wakwanza kukusema, kuchekwa na kutengwa mixer dharau!, kuwa na kiasi katika kusaidia pasipo kuathiri bajeti na mipango yako.
 
Mimi huwa najiambia tu, ‘mfano akikosa hii Pesa kutoka kwangu Je, atafariki dunia..!?’

then nikipata uhakika hatokufa, na upatikanaji wa hiyo Pesa haupo ndani ya uwezo wangu jibu ni moja tu ‘SINA’..!

sababu hata kama utoe figo yako uiuze kuna muda wewe bado utabaki tu mbaya kwenye simulizi zao, hakikisha sana hujiumizi ili kufurahisha watu ambao hata likitokea lolote kwako leo hawatohangaika na wewe kamwe na hata wakifanya ni zile siku mbili tu za mwanzo..!

FAMILIA YAKO, hicho ndiyo kiwe KIPAUMBELE chako..!

THE STREET FORGETS…!
 
Haohao ndio baada ya muda wataanza kukusema una kazi nzuri lakini huna maendeleo. Fanya maisha yako mkuu, ndugu hawana shukrani, wengi ni mahayawani tu
 
Kuna Mzee aliwahi sema Ukifadhili Ndugu Utavuna Magugu Mwishowe Uliwe Kibudu!
 
Back
Top Bottom