Ulikua unapenda kwenda na nini Shule hasa hizi za Msingi?

Ulikua unapenda kwenda na nini Shule hasa hizi za Msingi?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Shule za Msingi burudani sana kuna watu kila siku lazima mifuko ya Kaptula au sketi inatuna.

Wengine walikua wakija na mahindi ya kukaanga/Ruketo hapa palikua pazuri mwalimu anapiga pindi nyie mnatafuna mahindi ya kukaanga ngojea asikie harufu mtakataana.

wengine mahindi ya kuchoma kapuchukua katia kwenye mfuko au mzima mzima hivyo hivyo

wengine Sukari hapa wengi hii walikua wanaiba nyumbani sidhani kama wazazi walikua wanawapa tena enzi zile sukari ni kama jiwe la tanzanite.

wengine Maandazi/Mikate hapo utakuta mfuko umejaa mafuta tu

Hili wachache watakua wanalijua Kuna kitu ilikua inaitwa KONGO huu ni unga wa mahindi unalowekwa na kukaangwa kabla ya kupikia pombe ya kienyeji aina ya BUZA kuna mafundi walikua wanakuja nao unachanga na sukari kitu kinakua poa ila inabidi mlie nje ya darasa manake hiyo harufu yake ni hatari.

Wengine mpaka ukoko wa ugali aisee na bado wana wanaomba wapewe.

Wengine wanakuja na Pipi halafu hapo unakuta kakwapua pesa ya mzazi kikinuka anataja wote waliokula pipi viboko kwa sana.

Wengine mpaka Nyama za kukaanga,Bana bana ilikua powa haya mambo ya ubuyu sijui kashata,sijui barafu,popcorn hayakuwepo kabisaa.

Wewe mfuko wako wa kaptula/Sketi ulikua haukosi nini??

Twende kazi.
 
Alizeti kwenye mifuko ya kaptula.

chaa kuna mahali nimepita nikakuta ufuta umeota nikakumbuka stone age aisee tulikua tunakaanga Alizeti hii kitu ukikaanga ni tamuje ila watoto wa leo sidhani wanataka popcorn tu
 
chaa kuna mahali nimepita nikakuta ufuta umeota nikakumbuka stone age aisee tulikua tunakaanga Alizeti hii kitu ukikaanga ni tamuje ila watoto wa leo sidhani wanataka popcorn tu
Enzi zetu ilikuwa raha sana.

Siku moja mshikaji akamuomba mshichna mmoja alizeti msichana akamwambia imeisha, jamaa hakuamini akaambiwa hakikisha mwenyewe kwenye mfuko wa sketi.
Mshikaji alipoingiza mkono,nusura aifikie chumvini, Daaahhh msichana alibaki amepigwa na butwaaa tu.
 
Mayai na furu nilikua naenda kupiga sell kimya kimya.
 
kuna jamaa mmoja alikuwa anakuja sana na hela shuken kila cku xax cc tukanchora na uzembe wake anaziach kweny kibeg cha sport daah tunazibeba na kwenda kuzfukia kweny mchanga juu tunawek alama afu mwalim akija kutukagua sieee haaa hamn kitu
 
Z oo biskuti, zile zilikua na maumbo ya wanyama
Mango juice
na maji
 
Lazima niwe na kipande flan hivi cha kioo kwa ajiri ya kupigia chabo
 
Mfuko wangu wa marlboro au Ule wa gunia (salfeti)nahifadhia daftari zangu
 
Uketo,a.k.a mahind ya kukuaanga,ikifika saa nne madem wote wananitolea macho maana wanajua kuna tycun wa mahindi ndio muda wake wa kuonyesha jeuri
 
Alizeti kwenye mifuko ya kaptula.

Yaani we jamaa umeniwahi aisee. Kulikuwa na mwanangu kwao wanalima hizo bangayeye balaa. Nikimpitia kwenda shule nabeba za kutosha natia mfukoni. Basi hapo ni mwendo wa kutupia hadi skuli. Duh!! Those days bana [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Yaani we jamaa umeniwahi aisee. Kulikuwa na mwanangu kwao wanalima hizo bangayeye balaa. Nikimpitia kwenda shule nabeba za kutosha natia mfukoni. Basi hapo ni mwendo wa kutupia hadi skuli. Duh!! Those days bana [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2]
Darasa lilikuwa linageuka kama makazi ya panya
 
Back
Top Bottom