Ulikutana na changamoto zipi wakati unatafuta chumba au nyumba ya kupanga?

sic2019

Senior Member
Joined
Oct 14, 2018
Posts
129
Reaction score
81
WanaJF habari,

Poleni kwa harakati za kutafuta chochote kitu ikiwa ni moja ya majukumu ya kila siku.

Ndugu yenu nimeleta Uzi huu nataka niingie kwenye level ya kujitegemea na kumiliki gheto langu kwa hiyo nitafurahi sana mkinisaidia katika hili.

Niende moja kwa moja kwenye point kama kichwa cha Uzi kinavyosema ningependa kufahamu vitu vifuatavyo:-

1. Ningependa kufahamu changamoto zipi ulizipitia kipindi unatafuta nyumba au chumba cha kupangisha?

2. Na kipi ungependa kiboreshwe?

Naamini nitapata majibu yaliyo bora na sahihi kabisa kutoka kwenu.

Ahsanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkoa upi sasa mkuu maana changamoto zinatofautiana kulingana na maeneo, mfano hapa Dar madalali ni changamoto lazima wale kodi ya mwezi mzima hapo na wengine wanapandisha kodi wao kwa makubaliano na mwenye nyumba badae anafuata pesa yake.

Wengine maneno mengiii alafu nyumba mbovuuu basi tu akulie hela yako kwa udalali.

Ila kuna mikoa hakuna mtu anayeitwa dalali wala hawamjui ni nani sana sana watakuambia huyu "tapeli" hawajazowea kuona mtu asiye mwenye nyumba akiongelea nyumba kama yake.

Ni hayo tu mdogo wangu.

VIIXCCCL GrandLodge,ARUSHA
 
changamoto nyingi utakutana nazo baada ya kuhamia mahali, siku ya kwanza huwezi kuziona, kama umbea, kutonunua umeme, usafi, wizi uswahilini ukianika nguo lazima uichunge mpk ikauke, binafsi nakushauri tafuta nyumba yenye wapangaji wachache kuanzia wawili mpk watano, hapo utakuwa umepunguza kero nyingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changamoto ipo kwa madalali unamuelekeza nataka chumba/vyumba/nyumba ya namna hii, tuseme nataka nyumba iliyo karibu stand ya magari na nyumba ilipo gari ifike mpaka mlangoni.

Subiri uone hizo nyumba atakazo kupeleka tofauti na ulivyomuelekeza, halafu baada ya hapo anataka 5000 ya usumbufu [emoji28][emoji28]

Nimekuelewa mkuu kwahiyo kitu ambacho natakiwa kuzingatia pia ni idadi ya wapangaji kwa sababu inaweza ikapelekea kuwa kero hapo baadae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changamoto moja nlikutana nayo baada ya kuhamia hyo nyumba kumbe kulikua na deni/tatzo la umeme. So kila ukinunua umeme wanakata nusu then napata units za nusu yake mfano nikinunua wa elf 20, napata wa elf 10. Kuja kufatilia mwenye nyumba akagundua kuna deni kubwa waliokua wanakaa kabla kuna mambo yalifanya so wanakata hvyo had deni liishe.

So kabla ya kuhamia lazima umuhoji mwenye nyumba kama kuna deni lolote either dawasco au tanesco

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changamoto ipo kwa madalali unamuelekeza nataka chumba/vyumba/nyumba ya namna hii, tuseme nataka nyumba iliyo karibu stand ya magari na nyumba ilipo gari ifike mpaka mlangoni.

Subiri uone hizo nyumba atakazo kupeleka tofauti na ulivyomuelekeza, halafu baada ya hapo anataka 5000 ya usumbufu [emoji28][emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh kweli hili ni jambo LA kuzingatia mwanzoni kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changamoto moja nlikutana nayo baada ya kuhamia hyo nyumba kumbe kulikua na deni/tatzo la umeme. So kila ukinunua umeme wanakata nusu then napata units za nusu yake mfano nikinunua wa elf 20, napata wa elf 10. Kuja kufatilia mwenye nyumba akagundua kuna deni kubwa waliokua wanakaa kabla kuna mambo yalifanya so wanakata hvyo had deni liishe.

So kabla ya kuhamia lazima umuhoji mwenye nyumba kama kuna deni lolote either dawasco au tanesco

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana mkuu.
Kumbe mwenye nyumba anaweza akaficha baadhi vitu.
Duuh sasa mkalimaliza vipi hilo tatizo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku nilipo kabila letu lina sifa mbaya, kwa hiyo kupata chumba ilikua tabu, ikabidi nidanganye eti Mimi msukuma ndio nikapata chumba.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] wanazingua sana

Back
Top Bottom