Ulikuwa kiranja gani shuleni enzi unasoma msingi?

hahah,sijawahi kuwa kiranja ase wala monitor,though nlikuwa napenda sana ila nyota n bahati kipind iko sisi wengine tulikuwa ndo wasumbufu wa darasa,hatupo smart au hata huwa tunakuwa wa kwanza kutoka mwisho katika mitihani ase,ilikuaga magape san zaman primary school.teh
 
Daaaah kitambo kidogo.....shule ya msingi nliwahi kuwa monitor darasa la sita c, o level nyegezi seminary kuanzia form one B mwezi wa saba mpaka namaliza form four B nlikuwa monitor......nakumbuka visa vingi na vitimbwi vya seminari shukrani kwa mungu nlimaliza salama.
 
hahah,cijawah kuw kiranj ase wala monitor,sema nlikuwag napend san ila nyota n bhat kipind iko sis wengne tnakuwag nd wasmbuf w daras,hatpo smart au hat huw tnakuw w kwanz kutok mwshon ktika mitian ase,ilikuaga magape zaman prmary.teh
Kwa uandishi huu sidhani kama naweza kua peke yangu tu ambae nimeshindwa kuelewa ulichokiandika! Haraka ya nini Mkuu? Unawahi Treni?
 
Nilikuwa kiranja wa mazingira toka darsa la 4 mpaka namaliza shule ,form 2 nikawa kiranja wa mazingira tena mpaka namaliza form 4
 
Monita muandika wapiga fujo na mkusanya daftari za wanadarasa
 
Mashindano yaliendeshwa kwa njia ipi mpaka wewe ukawa Champion?πŸ˜€πŸ˜€
Mkuu nilichaguliwa kishsbiki maana asilimia 90 walinipa kura...Sasa ningumu kwa mpigaji kelele maarufu wa zamani kuwageuka wenzake...Mi nikawa siwaandiki majina ila ndio naungana nao kama genge moja la wapiga kelele..

Baada ya siku mbili za kuwa madarakani nikapinduliwa na ticha wa darasa
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kiranja wa nidhamu, nilikuwa nikiogopwa na wanafunzi kuliko hata baadhi ya walimu. Maruku sec hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…