Ulikuwa kiranja gani shuleni enzi unasoma msingi?


Ticha wa Darasa alikuwa Mwalimu Jecha au Mwalimu Lubuva?[emoji3][emoji3][emoji3]
 
kiranja wa ushuru....yaaan apo wamama wa maandaz walikuwa wananikoma full kula rushwa....jmn rushwa nimeianza mapema tangu std 4
 
O-level, mi kazi yangu ilikuwa nikuwatibua tu Viranja hasa wa dinning pamoja na walimu wao, nilikuwa nina kamati yangu hiyo kazi yetu kubwa shule ilikua ni kuiba "top layer" ya beans na kupiga ile misuli mirefu baada ya shibe with results Tembo. Mpaka tunamaliza hatukuwahi stukiwa. Ila walio jaribu kutuiga walipewa za chembe. Kwa kweli Idumu Top layer ilitusitiri sana.
 
Mimi nilipoanza shule siku ya kwanza nilichaguliwa monitor ya pili kiranja na siku ya tatu Mkuu wa Shule akaja na kunichagua nikawa Mwalimu kabisa niliupita ukiranja nikawa naamkiwa na kuchapa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
la tatu na lanne monitress la tano la sita kiongozi wa chakula la Saba Dada mkuu
 
Primary- kiongozi wa wapandisha Bender's
Alevel- montress na waziri wa starehe
Chuo- mbuge wa darasa
 
nilikua kiranja wa watoro....ilikua huwezi kudoji kipindi au kwenda kijijini kama sina habari zako
 
Kiranja wa nidhamu from form two to 4, advnc nilipita patupu, chuo nilikua fucult Representative for three years
 
Daaah nakumbuka darasa la tatu nilichaguliwa kuwa kiranja wa usafi ,sasa taabu ilikuwa inakuja pale mwalimu wa zamu anapokwambia ukawazuie wachelewaji.Nilikuwa napata shida sana maana darasa la sita na la saba walikuwa ni wa baba wenye familia zao ukimsimamisha unafanya kumwambia bro naomba kesho ujitahidi kuwahi ,baadae mwalimu akikuuliza ulio wakamata unabaki kujiuma uma mdomo.
 
Darasa 1-3 kiongozi wa darasa, darasa la 3 hadi 4 kiranja wa kawaida. Na pia wa taaluma. Dara 4 hadi 5, kaka mkuu msaidizi; Darasa la 5 hadi la 7, Head prefect kamili. Nikiweka rekodi ya head prefect mdogo na aliyeshika cheo hicho kwa muda mrefu kuliko wote. Drs la 1 hadi 7 sijaiachia namba moja. Form 2, waziri wa Elimu.
 
mi nilichaguliwa kiranja mkuu for over 80% ya vote za wanafunzi..... ila waalimu wakanigomea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…