Ulikuwa wapi wakati Ufaransa hii inaitoa nishai Italy Euro 2000

Ulikuwa wapi wakati Ufaransa hii inaitoa nishai Italy Euro 2000

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Nyakati ngumu hazipiti ila watu wagumu wanapita. Pata picha jinsi Ufaransa hii ilivyosheheni katika michuano ya Euro 2000.
1.Barthez
2.Lilian Thuram
3.Bixente Lizarazu
4.Laurent Blanc
5.Marcel Desailly
6.Patrick Viera
7.Robert Pires
8.Youri Djokaeff
9.Thiery Henry
10.Zinedine Zidane
11.Sylvan Wiltord

Sub:
David Trezguet
Christoph Dugarry
Patrick Karembeu
Emmanuel Petit
Frank Libouf

Hapo captain Didier Deschamps alishastaafu.

Hakika sidhani kama Wafaransa watakuja kupata kikosi mahiri kama hiki, timu ilienea haswa! Hapo Fainali Italy anakufa kwa goli la dhahabu, Nyakati zimekwenda wapi? Ulikuwa wapi wakati kikosi hiki cha Les Bleus kikitikisa Ulaya na Dunia nzima?
 
Kitambo sana mkuu, hapo ndio hasa mpira ulikuwa damuni.. kila nikimchek zidane, hapa henry kichogo aisee hili chama likinikosha, na kichogo ndio alinitia kwenye matatzo ya kuipenda arsenal..

Ila mkuu nakumbuka Deschamps alikipiga hayo ndio mashindano yake ya mwisho baada ya hapo akatundika daruga
 
Ungerudi nyuma kidogo 1998 World Cup Ufaransa akiwaua mabingwa wa kihistoria Brazil pale Stade de France.Zidane anatupia mbili na Emanuel Petit anamalizia goli la tatu baada ya kumpoteza kipa bora kabisa Tafarel.
Bonge la game. Ni Ufaransa hii ambayo baada ya kuchukua World cup, ikachukua Euro na Confederation cup. Kikosi bora kabisa ambacho hakijatokea tena kwa nchi ya Ufaransa. Spain ikaja ikafanya vile vile, world cup na Euro .

Kikosi kamili Barthez, Thuram, Desailly, Lebouef, Lizarazu, Deschamps, Petit, Karembeu, Zidane, Djorkaeff, Guivarc’h Subs – Vieira, Boghossian, Dugarry
Ufaransa hii inarudi kwenye fainali miaka minne baadaye 2002 na kuishia hatua ya makundi. Mechi ya ufunguzi kundi A ikikutana na Senegal yenye kikosi cha dhahabu. Ufaransa wanakufa goli 1 kwa sifuri, Zidane akiwa majeruhi kwenye benchi.
Ufaransa hii ikajaribu kurudi tena 2006 na kuishia fainali dhidi ya Itali iliyosheheni vipaji chini ya kapteni Canavaro.
 
Hakuna Mechi Iliniuma kama Fainali ya Euro 2000 nilikuwa siwapend France toka Alivyowafunga Brazil 1998 na akaja fainali akampiga Italy
Italy wanapata Goli Wiltord anaswazisha ngoma inaenda Extra Time
Trezeguet anapiga Bonge la Goli Extra Time.
 
Yaah trezagoal na kale kamzuzu kake ka kiushkaji mtoto wa jorge Ernesto Trezeguet beki wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina.
 
Kitambo sana mkuu, hapo ndio hasa mpira ulikuwa damuni.. kila nikimchek zidane, hapa henry kichogo aisee hili chama likinikosha, na kichogo ndio alinitia kwenye matatzo ya kuipenda arsenal..

Ila mkuu nakumbuka deschamps alikipiga hayo ndio mashindano yake ya mwisho baada ya hapo akatundika daruga
Paragraph ya I kuna kitu umesema, siri yangu na maumivu yangu!
 
hapana chezea chogo a_k,a henry huyu kuna bwana kuna rekodi ameweka na bado haijavunjwa bwana chogo alikuwa akipiga kona zinajaa moja kwa moja kwenye nyavu pia ile staili ya driboling ya mpira bado hakuna aliyeweza kumfikia
Kaivunja kichuya bwana
 
Nyakati ngumu hazipiti ila watu wagumu wanapita. Pata picha jinsi Ufaransa hii ilivyosheheni katika michuano ya Euro 2000.
1.Barthez
2.Lilian Thuram
3.Bixente Lizarazu
4.Laurent Blanc
5.Marcel Desailly
6.Patrick Viera
7.Robert Pires
8.Youri Djokaeff
9.Thiery Henry
10.Zinedine Zidane
11.Sylvan Wiltord

Sub:
David Trezguet
Christoph Dugarry
Patrick Karembeu
Emmanuel Petit
Frank Libouf

Hapo captain Didier Deschamps alishastaafu.

Hakika sidhani kama Wafaransa watakuja kupata kikosi mahiri kama hiki, timu ilienea haswa! Hapo Fainali Italy anakufa kwa goli la dhahabu, Nyakati zimekwenda wapi? Ulikuwa wapi wakati kikosi hiki cha Les Bleus kikitikisa Ulaya na Dunia nzima?
Captain yupo bench mkuu?

Simuoni hapo Stephanie Guivarc'h mtaalam...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo Nko Darsa La Pili. Nimetoka Kuangalia Michuano Yangu Ya Kwanza Ya Africa 2000 Januari,Tunaangalizia Bar Ya Jirani. Ndipo Nlipokuja Kuambiwa Kuna Euro Dogo Mechi Ya Kwanza Naona Mfaransa Anakufa Kwa Mholanzi,Alafu Nikaja Kuona Mholanzi Anakufa Kwa Muitaly Na Mipenalt Wakakosa Kama Vipofu. Nakuja Kuchukuliwa Fainali Nakuta Mfaransa Niliyemuonea Huruma Na Kufadhaika Anacheza Na Italy. By The Way Enzi Hizo Timu Ikivaa Blue Au Kijani Tu Inakua Timu Yangu Automatically,So Italy Walivyovaa Jezi Nyeupe Fainali WakajiDisqualify Wenyewe. Hapo Ndo Nkaanza Na Kushika Majina Ya Wachezaji Na Kuwajua Maana Nlikua Nawaona Katika Stickers Tu Tulizokua Tunabandika Katika Madaftari,Ndo Kuona Huyu Zidane,Huyu Barthez!
Waitaliano Wameshikana Mabegani Wanashangilia Huku Nje Ila Sylvain Wiltord Had Other Ideas,Chwaaaaaaaaaaah! Fransesco Toldo Anakuja Kubana Miguu Nyavu Zinatikisika.
Kusema Ukweli Enzi Hizo Age Mates Na Marafiki Zangu Walikua Hawaelewi Kitu Kuhusu Football,Wao Uwaekee Bruce Lee Na Komando Kipensi.
Nawashukuru Sana MaBroo Zangu Kwa Kunitambulisha The Second Thing I Love The Most After My MOM!
 
Back
Top Bottom