Ulilipokea vipi shambulio la JF?

Ulilipokea vipi shambulio la JF?

Niwe mkweli na sihitaji mtu aniamini mimi nilifanya kolabo na tunguli kwahiyo nikawa online muda wote... Shida ni kwamba sikuwa na wakuchat naye.. Hivyo nikawa navinjari tu majukwaa yasiyo na watu kama wale manjagu leo mitaani
hahaha
 
Kuna wasiosali walisali jana
Sio kwa kuhangaika huko utafikiri umepoteza funguo za nyumba ndani ya simu unavyozitafuta hahahaha
Kila sekunde unachungulia utafikiri umeahidiwa unatumiwa hela halafu unashida kinoma hahaha

Yani kila baada ya dakika kadhaa mtu lazima uchungulie humu halafu unakuta hewa hahahaha
 
Kwa mara ya kwanza nilijua bando limekata, kucheki nina gb kama zote hivi, nikajaribu tena naona mambo yanazunguka tu, nikadhani ttcl wananiletea mambo meusi, nikajaribu kutrmbelea sites nyingine naona ni kitonga tu, akili ikagonga kichwani nikajua hapa kuna kitu aidha mkuu ndio kaishafungia mitandao yetu au kuna jitu linataka kuhack akaunt yangu , kuchungulia mahala fulani ndio nikapata habar kuwa jf imeshambuliwa.
 
Back
Top Bottom