Ulimi kuungua

Ulimi kuungua

Daata

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
4,673
Reaction score
1,875
Heshima kwenu wanajukwaa.

Nina tatizo ambalo nimekaa nalo kwa kipindi kirefu nikidhani kuwa ni jambo la kawaida.
Tatizo langu ni ulimi kuungua kila ninapokula/kunywa kitu chochote cha moto. Ni tatizo ambalo nimekuwa nalo kwa miaka mingi.
Tukikaa na mtu tunakunywa chai ninatumia muda kiasi kwamba huyo mtu anaweza kunywa hata vikombe viwili mi bado nahangaika na kimoja.
Hapa nilipo ulimi una viraka baada ya kuungua vyenye kufanana na ramani sijui ya nchi gani.
Kuungua huko hakutengezi kidonda japokuwa huuma isipokuwa sehemu ya juu ndiyo huungua na kuonesha utofauti na sehemu zilibakia lakini baada ya muda kama siku tatu ulimu hurudia hali yake na hivyo viraka hutoweka na maumivu pia hutoweka.

Naomba kujuzwa mwenye ufahamu wa hili tatizo.
 
Pendelea kula vyakula vya baridi uasipend kula vyakula vya moto kwa mfano chai kunywa iwe ya uvuguvugu usinywe chai ya moto sana na uwe unajipaka asali kwenye ulimi wako utapona.
 
Mmmh! hiyo asali kwenye ulimi itakaa? si ataimeza tu
 
Pole mwaya... usinywe vtu vya moto sana..... umenichekesha uliposema una ramani na hujui ya nchi gani.... natamani kama ungeweka picture ni kwambie.. maana nahisi itakuwa ramani ya visiwa vya Madagascar
 
Pendelea kula vyakula vya baridi uasipend kula vyakula vya moto kwa mfano chai kunywa iwe ya uvuguvugu usinywe chai ya moto sana na uwe unajipaka asali kwenye ulimi wako utapona.

Asante kwa ushauri
Inafika wakati natamani niombe glasi ya ziada kwa ajili ya kupoozea kawa mtoto mdogo nikiwa napata chai.
 
Wakati bado nipo kijana miaka kama 25 nilikuwa na tabia kama yako nikipata chai ya moto ninakunywa pasipo na kusubiri ipowe Marehemu mama yangu akanikataza nisifanye hivyo nikaacha mwenyewe kufanya hivyo sasa na wewe jiepushe kula au kunywa chai au vitu vya moto kwanza havina baraka vikiingia tumboni kwa sababu ya umoto wake pili utadhurika baadae na maradhi usiyoyategemea mwilini mwako kuwa muangalifu sana.
 
Back
Top Bottom