Ulimi ni kiungo kinachoweza kukujenga au kukuangusha

Ulimi ni kiungo kinachoweza kukujenga au kukuangusha

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ulimi ni kiungo kidogo ambacho hutusaidia kumezea chakula pia hutusaidia kutamka maneno na kuwa na mawasiliano na viumbe wengine.

Ulimi ni kiungo cha muhimu sana. Ni gate kati ya yaliyo moyoni mwako na dunia. Ukidhibiti ulimi hakuna atakae jua yaliyo moyoni mwako. Labda uyaandike.

Ulimi ni kiungo ambacho hakina mfupa lakini kimewekewa walinzi 32 wa kukilinda. Ulimi unaweza kukupatia heshima na marafiki kama utautumia vizuri. Kinyume chake ulimi unaweza kuku dharaulisha na kukujazia maadaui.

Tuwe makini na matumizi ya kiungo hiki, shirikisha viungo vingine kama moyo na ubongo kabla hujatumia ulimi sikuzote.
 
Wanakitumia vibaya sana hiki kiungo maskini wanakilambisha hadi chumvichumvi!
 
Attachments

  • IMG-20171108-WA0005.jpg
    IMG-20171108-WA0005.jpg
    56.6 KB · Views: 42
Ulimi ni kiungo kidogo ambacho hutusaidia kumezea chakula pia hutusaidia kutamka maneno na kuwa na mawasiliano na viumbe wengine.

Ulimi ni kiungo cha muhimu sana. Ni gate kati ya yaliyo moyoni mwako na dunia. Ukidhibiti ulimi hakuna atakae jua yaliyo moyoni mwako. Labda uyaandike.

Ulimi ni kiungo ambacho hakina mfupa lakini kimewekewa walinzi 32 wa kukilinda. Ulimi unaweza kukupatia heshima na marafiki kama utautumia vizuri. Kinyume chake ulimi unaweza kuku dharaulisha na kukujazia maadaui.

Tuwe makini na matumizi ya kiungo hiki, shirikisha viungo vingine kama moyo na ubongo kabla hujatumia ulimi sikuzote.

Dadangu Sky Eclat , Biblia haijaacha kitu, hebu soma hapa kitabu ya Yakobo (my favorite Book)
Yakobo 3:5-10

5 Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.
6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.
7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.
10 Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
 
Kiungo ambacho kikitengemaa bas mambo huwa mazur na kiki haribika hatari huepo
 
Back
Top Bottom