Ulimwengu wa digitali ni changamoto kwa magazeti

Ulimwengu wa digitali ni changamoto kwa magazeti

Miaka kadhaa iliyopita kabla ya kuja kwenye digitali watu walilazimika kununua magazeti kwa sababu nyingi tofauti tofauti, jambo kubwa halikuwa kupata habari kujua yanayoendelea pekee

Sababu za kununua magazeti
Kwanza ilikuwa kuhabarisha lakini pia kujua matangazo ya serikali kama zabuni au minada, pia ilikuwa zitokea teuzi au watumishi kupata kitu fulani basi magazeti yalitumika

Vijana walinunua magazeti kuangalia nafasi za kazi au kutafuta wachumba(Pen Pals)

Wanafunzi walihitaji magazeti ili kupata mitihani au kupata majibu ya mitihani waliofanya

Kwenye ulimwengu wa digitali, habari inapatikana na kusambaa mara tu baada ya kitu kitokea, au ukitaka kukijua vizuri unaweza kuingia mitandao kama jamiiforums.com ukapata habari kiundani na sio kusubiria kesho yake, mambo mengi hufanyika kwenye websites husika, ajira zinapatikana kwenye portals, mitihani inapatikana kwenye apps na mengine mengi yamebadilika

Nini Kilifanyika
Hali hii ililazimisha magazeti kuwa na websites ili kuwahabarisha wateja wake, lakini websites ni gharama kwa anayeiendesha, Kwa ulimwengu wa sasa website inaongeza jina lakini ziko changamoto kadhaa katika nafasi hiyo

Kifupi naona usomaji wa magazeti umepungua kwa kuwa watu wamehamia kwenye ulimwengu wa digital

Baadhi ya makampuni yaliuza magazeti mtandaoni kupitia apps ili mtu aweze ku-subscribe na kupata huduma, lakini wabongo tabia za kununua vitu ni duni sana, fikiria kama mtu anataka antivirus ya bure anaweza kutoa hela kununua habari wakati anaweza kuisoma twitter nk, lakini pia walioko mtandaoi hawajui kuhusu vitu vingi vya mtandaoni na hii huleta changamoto nyingine

SULUHU NINAYOIONA

Kutokana na kuathirika kimapato magazeti yawe biashara huria, kusiwe na malipo serikalini ili kuwawekea uwanja mzuri wa watu kushindana katika kuhabarisha na kuburudisha

Badala ya kusaka habari, magazeti yawe ni ya kutoa vitu vyenye fikra(Makala) kwa kuwa katika uwanja huo ndio watu wanaeza kuona haja ya kununua, mnakumbuka umaarufu wa magazeti yaliyokuwa na makala zaidi kuliko habari kama Mwanahalisi, Tazama Tanzania, Rai, nk

NB: Maelezo haya hayatokani na tafiti bali yanasimama kama hypothesis
Umejaribu kutengeneza kitu mutokana na hypothesis yako endelea kyifanyia kazi na katika kufanya hivyo utafiti wako uangazie hali ya kisiasa ilivyo athiri sekta ya habari,kwa kutazama sheria mpya na utashi wa kisiasa.
 
Nasikitika kuna jambo noja ambalo watu wengi mnashindwa kulijua nalo ni Matangazo.

Kitu pekee kinachoendesha kampuni ya magazeti n matangazo, lkn tangu mzee baba aingie ameelekeza kwamba taasisi zote za Umma n lazma zitoe matangazo yake kupitia magazeti ya serikali "Daily News na Habari leo"

Hivyo private sector kwa kiasi kikubwa sana wameathirika na hili na kupelekea kupoteza mapato mengi sana.

Naomba tu niseme nakala (copies) hazijawahi kuwa na mauzo ya kutosha kuwezesha kuendesha kampuni.
 
Kinachoua biashara ya magazeti sio technology bali kukosekana kwa ueledi, watu walununua magazeti ili wapate habari na makala za uchambuzi ila kinachofanyika awamu hii ni kuandika ngonjera na makala za kusifia watawala, wanapaswa kujifunza kwenye magazeti kama east african
 
Sasa hivi ni zamu ya kwenda kula ulikopeleka mboga,
Uchaguzi umeisha,
Wenye vyombo vya habari,waambieni mliokuwa mnawaimbia mapambio ,kuwasifu na kuabudu, ndiyo wanunue magazeti yenu,nk.
 
Back
Top Bottom