Ulimwengu wa digitali ni changamoto kwa magazeti

Umejaribu kutengeneza kitu mutokana na hypothesis yako endelea kyifanyia kazi na katika kufanya hivyo utafiti wako uangazie hali ya kisiasa ilivyo athiri sekta ya habari,kwa kutazama sheria mpya na utashi wa kisiasa.
 
Nasikitika kuna jambo noja ambalo watu wengi mnashindwa kulijua nalo ni Matangazo.

Kitu pekee kinachoendesha kampuni ya magazeti n matangazo, lkn tangu mzee baba aingie ameelekeza kwamba taasisi zote za Umma n lazma zitoe matangazo yake kupitia magazeti ya serikali "Daily News na Habari leo"

Hivyo private sector kwa kiasi kikubwa sana wameathirika na hili na kupelekea kupoteza mapato mengi sana.

Naomba tu niseme nakala (copies) hazijawahi kuwa na mauzo ya kutosha kuwezesha kuendesha kampuni.
 
Kinachoua biashara ya magazeti sio technology bali kukosekana kwa ueledi, watu walununua magazeti ili wapate habari na makala za uchambuzi ila kinachofanyika awamu hii ni kuandika ngonjera na makala za kusifia watawala, wanapaswa kujifunza kwenye magazeti kama east african
 
Sasa hivi ni zamu ya kwenda kula ulikopeleka mboga,
Uchaguzi umeisha,
Wenye vyombo vya habari,waambieni mliokuwa mnawaimbia mapambio ,kuwasifu na kuabudu, ndiyo wanunue magazeti yenu,nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…