Bila shaka mmekusanya vitu vyote nilivyoainisha hapo juu, sasa twende kazi.Unganisha ungo wako vizuri na hakikisha pale utakapoliweka pako level,umewaka kisabuni (neflon) kwenye cband lnb na uifunge kwenye dish vizuri, weka pins kwenye cable na ncha moja iungwe kwenye lnb na nyingine kwenye receiver.
Fungua receiver yako na uweke tp hizi 3642 H 8545(kama cable imeungwa vizuri utaona mstari mwekundu kwenye screen yako).Elekeza ungo wako kuelekea mashariki (angalia ungo wa jirani yako).Kwa kutumia rula yako pima nguzo ya nyuma ya ungo 25-30cm weka alana fix kwa kutumia screw inayoonekana hapo.
Tuanze kuzungusha ungo,anza kwa kuzungusha kitako cha ungo na wakati unafanya hivyo hakikisha unaangalia kwenye screen yako,utaona ule mstari mwekundu unaongezeka asilimia na acha kuzungusha pale utakapojiridhisha kuwa mstari mwekundu hauongezeki tena.
Sasa rudi kwenye ile screew nyuma ya dish ifungue na elevate or lower dish lako, utafika pointi ambayo utaona kuna mstari mwingine wa kijani umetokea.hapo utakuwa umeipata satellite ya intelsat906 scan kupata channels zako za IPP Media. ukiona haijatokea mistari hiyo toa H na weka V na urudie zoezi lako.Nakaribisha mijadala.