sijui nini
JF-Expert Member
- Sep 29, 2010
- 2,553
- 1,291
Dish langu ni la futi 6, LNBF ni C-Band, Receiver ni media Com MFT 910+New. Nilifanikiwa ku-install local channels ITV(na ndugu zake), Star TV,TBC1. Tatizo radio zake sizipati? Pili, nimenunua LNB ya pili C-Band, naomba kanuni za kuifunga na frequency zilizo upande mmoja na aljazeera. Tatu, ninashindwa kupata channel ten. Ahsante.
kuna mediacom ambazo hazina progam ya radio ambayo ina taa nyekundu bila shka ya kwako ipo hivyo
Nilishawahi kutumia tumia mediacom 910 new receiver, yenyewe ina sapoti radios.chagua channel mfano tbc1 na bonyeza kitufe cha audio,chagua audios zinazoonekana.
Bila shaka mmekusanya vitu vyote nilivyoainisha hapo juu, sasa twende kazi.Unganisha ungo wako vizuri na hakikisha pale utakapoliweka pako level,umewaka kisabuni (neflon) kwenye cband lnb na uifunge kwenye dish vizuri, weka pins kwenye cable na ncha moja iungwe kwenye lnb na nyingine kwenye receiver.
Fungua receiver yako na uweke tp hizi 3642 H 8545(kama cable imeungwa vizuri utaona mstari mwekundu kwenye screen yako).Elekeza ungo wako kuelekea mashariki (angalia ungo wa jirani yako).Kwa kutumia rula yako pima nguzo ya nyuma ya ungo 25-30cm weka alana fix kwa kutumia screw inayoonekana hapo.
Tuanze kuzungusha ungo,anza kwa kuzungusha kitako cha ungo na wakati unafanya hivyo hakikisha unaangalia kwenye screen yako,utaona ule mstari mwekundu unaongezeka asilimia na acha kuzungusha pale utakapojiridhisha kuwa mstari mwekundu hauongezeki tena.
Sasa rudi kwenye ile screew nyuma ya dish ifungue na elevate or lower dish lako, utafika pointi ambayo utaona kuna mstari mwingine wa kijani umetokea.hapo utakuwa umeipata satellite ya intelsat906 scan kupata channels zako za IPP Media. ukiona haijatokea mistari hiyo toa H na weka V na urudie zoezi lako.Nakaribisha mijadala.
upo lacation gani kaka? W3C inapatikana vizuri sana kwa offset dish la angalau 75cms. Sijui jinsi ya kuposti pics tu ningekupostia beam hapa na pics mbalimbali za aligments za nyungo(naomba mnipe somo)Hiyo sat ya w3c 16 e bem yake inafika hapa bongo ? Je dish saizi gani ?
Kaka naona umeanza kunielewa.
Naomba u2mie hiyo asiasat105 kupata chaneli za bongo.Ikamate kwanza hiyo aljazeera, halafu kiweke kile kisabuni kwenye lnb, weka tp hizi 3642 H/V 8545 fungua ile screw iliyoko nyuma ya ungo na lower dish lako kidogo sana kwa angalau 4cm kupata signal.
Unaweza substitute H for V. (unapopima cm 30 kwenye nguzo ya nyuma...ni ipi?) Ni ile ya juu na upime kutoka juu na ufungie screew pale utakapowekea alama
upo lacation gani kaka? W3C inapatikana vizuri sana kwa offset dish la angalau 75cms. Sijui jinsi ya kuposti pics tu ningekupostia beam hapa na pics mbalimbali za aligments za nyungo(naomba mnipe somo)
shukrani sana kaka, umeniokoa sana..hivi nikitoka tu kwa ofisi nikifika kitu cha kwanza ndo hiyo kazi...hopefully nitaleta majibu kesho!! i hope it will work...thank u sana!
kaka hata mi niko moro mzumbe chuo kikuu.
Mi hizo startv, nmezkosa bana, almanusra nivunje kiuno juu ya bati!
Hivi upande wa kulia au kushoto wa Cband nikiweka lnb tapata channel zipi kwa position hii ya locol tvs?
Je kuna channel zozote za fta zinazoonyesha mechi za mpira wa ngazi yoyote kutoka South America? Kama zipo ni kwenye satellite gani na frequency zipi?