Mavella " nimepata chaneli 2 za bay TV na 1kzn TV kutoka south afrika ambazo ziko amos 5 at 17e ktk mwelekeo huohuo wa eutelsat 16A at 16e bila kusogeza dish "
Bro Mavella naomba ujaribu kuzungusha LNB @ 3:00pm ( namaanisha pale kwenye fitting ya cable panakuwa at 3:00pm ukiwa mbele ya dish lako )
Nina dishi la 6ft napata chaneli za bongo.Nataka kuweka lnb ya ku nipate za south africa na nollywood.Naomba kujua nitaiweka wapi na nahitajika ninunue vifaa gani.Kama kuna picha tafadhali naomba nione vipi lnb ya ku inakaa.
Njia ya pili ni kununua dvb-s2 decoder na offset dish la >3ft ili kukufanya unase sats eutelsat/amos ambapo utapata channels nyingi za sports zikiwemo rdv, drtv,rst1 ortb setanta africa na crtv
Thaicom 5 at 78.5KU mawimbi yana patikana huko tanzania esp dar .. naagiza hii kitu toka chinaAliexpress.com : Buy Premier League satellite receiver,Thaicom 5 at 78.5KU , 1 year subscription Enjoy world of knowledge and fan from True Visions from Reliable Premier League suppliers on satellite TV/dish /auto mobile antenna/decoder receiver kwa ajili ya wadogo zangu but inahitaji hizo frequency
Nashukuru kwa elimu yako na uendelee na moyo huo ni wachache wenye kutoa elimu ya namna hiyo
Mungu akupe kila la kheri na akupe ujuzi zaidi ili wengi wanufaike toka kwako
Thaicom haina coverage ya ku-beam hapa kwe2 na maeneo karibuni yote africa
Arselona na wengine wanaoweza kunisaidia. Naona swali langu limekuwa gumu maana nimeuliza mara nyingi sana humu bila majibu?
Ninatumia receiver/decoder ya Humax 2000 HD lakini nakutana na changamoto hii ambayo sikuwa nakutana nayo kwenye mediacom:
Nina shida mbili kubwa:
1. Channel mbili za tbc1 na star tv zinaingia kwenye channel moja. Yaani nikiweka star tv hiyo tbc1 inaondoka na star tv inakaa kwenye nafasi ambayo ilikuwa na tbc1 na, nikiweka tbc1 basi star tv inaondoka kwenye nafasi hiyo hiyo na tbc1 inakaa hapohapo. Sipati shida kama hiyo kwa station zingine. Sasa hapo nifanyeje ili zote ziwepo na ziwe na channel yake kila moja?
2. Sipati kabisa Channel ten. Nikii search siipati nikijaribu kuweka frequency zake naona signals kama zinaingia na kutoka (Unstable) na haipatikani. shida yaweza kuwa ni nini?
Mwisho nakili kwamba Arselona umekuwa msaada sana kwa watu wengi hapa na inaonekana unafahamu vizuri kitu hii. Asante.
Mavella Mpaka naleta hoja hapa ni kwamba nimeshajaribu kuweka moja moja na nikiweka moja moja napata matokeo niliyoainisha hapo mwanzo! Labda nijaribu kufanya hiyo unayosema ni restore settings lakini nikianza tena kufanya set up si nita end up na matokeo yale yale? Anyway ngoja nijaribujaribu kufuta frequency za tbc na star na uingize manual moja moja hii inawezekana ni kwasababu VPID na APID za tbc na star zinafanana ikishindikana fanya restore setting.
Hiyo sat ya w3c 16 e bem yake inafika hapa bongo ? Je dish saizi gani ?
Mkuu Eutelsat w3c 16A at 16.0°E KU BAND inapatikana Bongo (Tanzania) lakini inategemea uko wapi,pamoja na kuwa na beam ya South na East Africa...Inapatikana kwa dish la ukubwa wa 130cm- 80cm mikoa ya kusini,magharibi na mashariki na mpaka katika ya Tanzania mikoa ya kaskazini pengine kwa dish kubwa zaidi ya niliyo tangulia kuyataja lakini beam yake inaishia katikati ya Tanzania.
Kwa kuongeza ni rahisi kupata satelite ya Eutelsat 7A at 7°E na hata channels zake nyingi ni nzuri ni pia ukitazama beam yake kwa Tanzania nzima kwa dish la ukubwa wa 85cm.
Kama ukiweza kutumia motorized Dish kuanzia Eutelsat 7A at 7°E kuelekea East unaweza kwenda mpaka Nigcomsat 1R / Turksat 42° ........ukirudi ulipoanzia Eutelsat 7A at 7°E kuelekea West unaweza kwenda mpaka Telstar 11N (Telstar 11R) 37°W......kwa maana hiyo ukitumia Dish lenye motor unaweza kupata satelite zaidi ya kumi kwa wakati mmoja,mfano Turksat pekee yake unaweza kupata channels zaidi ya 130 za bure.
Mkuu tongoni dish la moto unamaana gani?