Mkuu Eutelsat w3c 16A at 16.0°E KU BAND inapatikana Bongo (Tanzania) lakini inategemea uko wapi,pamoja na kuwa na beam ya South na East Africa...Inapatikana kwa dish la ukubwa wa 130cm- 80cm mikoa ya kusini,magharibi na mashariki na mpaka katika ya Tanzania mikoa ya kaskazini pengine kwa dish kubwa zaidi ya niliyo tangulia kuyataja lakini beam yake inaishia katikati ya Tanzania.
Kwa kuongeza ni rahisi kupata satelite ya Eutelsat 7A at 7°E na hata channels zake nyingi ni nzuri ni pia ukitazama beam yake kwa Tanzania nzima kwa dish la ukubwa wa 85cm.
Kama ukiweza kutumia motorized Dish kuanzia Eutelsat 7A at 7°E kuelekea East unaweza kwenda mpaka Nigcomsat 1R / Turksat 42° ........ukirudi ulipoanzia Eutelsat 7A at 7°E kuelekea West unaweza kwenda mpaka Telstar 11N (Telstar 11R) 37°W......kwa maana hiyo ukitumia Dish lenye motor unaweza kupata satelite zaidi ya kumi kwa wakati mmoja,mfano Turksat pekee yake unaweza kupata channels zaidi ya 130 za bure.