Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu ni ndege gani na anapatikana wapi?
Wanagombana au wanacheza Ngoma????
huyu kiumbe anaitwa nani?
Asante sanaJe wajua!
Katika jamii za Ndege wengi, jinsi ya kiume ndio inakuwa na rangi nzuri za kuvutia kuliko jinsi ya kike. Mfano mzuri ni Tausi ambapo wengi tunafahamu uzuri wa mkia wake, usije jichanganya kuzani yule ni jike, la hasha yule ni kidume.
Katika nadharia za "Evolution of species" Inatoa sababu kwa nini jinsi ya kiume inavutia kuliko jinsi ya kike. Evolution hufafanua kwamba Katika jukumu kuu la kuendeleza kizazi jinsi ya kike katika jamii ya ndege ndio huchagua baba wa watoto. Sababu kuu inayowapa kiburi hiki ni kutokana na wao kufanya uwekezaji mkubwa katika mayai tofauti na jinsi ya kiume ambao uwekezaji wao katika mbegu ni mdogo mno: ushawahi sikia faster kama bao la Jogoo. Hivyo ni jambo la busara jike kutilia maanani nani atamtagisha, jike mwenye akili atataka Jogoo wake awe na afya ili wototo wake pia wawe na afya na waweze kupambana na maisha. katika njia jike atatumia kumtambua Jogoo mwenye afya ni kutokana na rangi zake!
Kutokana na sababu hio majike ndio wanachagua yupi atamtagisha, wanaume warembo wenye kuvutia ndio walikuwa wanapata nafasi ya kuchaguliwa na majike hivyo baada ya vizazi na vizazi wakawa wanaendelea kubadilika na kuvutia taratibu kulingana na ushindani. Hivyo ndivyo ikawa.
ACT members?