MTAZAMO WA KIFALSAFA KUHUSU ULIMWENGU WA MWILI NA ROHO
Kifalsafa, na hasa kwa mujibu wa Plato, maneno ulimwengu wa roho ni kinyume cha maneno ulimwengu wa mwili. Plato anaongelea "sensible world (ulimwengu wa mwili)" dhidi ya "intelligible world (ulimwengu wa roho)." Katika sulimwengu wa mwili, tunapata maarifa kwa kutumia milango mitano ya fahamu--kuona, kunusa, kusikia, kulamba, na kugusa.
Na katika ulimwengu wa roho tunapata maarifa kwa njia tatu kuu. Kwanza, kuna kusafiri katika barabara kwa kuanzia kwenye upande wa ushahidi mpana kuelekea upande wa ushahidi mwembamba (deductive reasoning).
Pili, kusafiri katika barabara kwa kuanzia kwenye upande wa ushahidi mwembamba kuelekea upande wa ushahidi mpana (inductive reasoning).
Tatu, kuna kusafiri katika barabara mbili zilizo sambamba huku ukiwa unafananisha yale unayoyaona katika barabara hizo mbili (analogical/analytical reasoning).
Na njia ya nne, ambayo haikubaliki tangu mapinduzi ya kisayansi yalipobisha hodi duniani, ni ile ya ndoto na maoni. Ndoto ni maarifa yasiyoweza kuthibitika wala kukanushwa, ama na mtu yule yule aliyeota, au watu bado. Kwa maneno mengine ni ushirikina.
Kwa hiyo, hivi leo, maneno ulimwengu wa roho yanamaanisha ulimwengu wa akili inayofanya kazi kwa mujibu wa kanuni za kimantiki. Kanuni hizi ni za makundi matatu--inductive logic, deductive logic and analogical/analytical logic. Hilo ni somo rasmi katika vianga vya falsafa.
Hivyo, wale jamaa wanaosema kuwa wanaingia katika ulimwengu wa roho kwa njia ya ndoto na maono, lakini sio kwa kupitia kanuni za mantiki (logic), ni washirikina kama sio matapeli. Na wale wanaoyakubali yale wanayoambiwa na huyo anayedai kuota kuhusu yaliyoko katika ulimwengu wa roho ni wajinga. Wanahitaji kukombolewa.
Kilichowapata ni collective imbecilisation, yaani wamefanywa kuwa halaiki ya misukule inayoweza kuamurishwa ifanye inavyoagizwa, kila wakati na kila mahali. Huo ndio mtazamo wa kifalsafa kuhusu swali "ulimwengu wa roho ni kitu gani?"
Na kuhusu habari ya kifo, kisayansi tunasema hivi: Kifo ni tukio ambamo mwili wa kiumbe hai unapoteza nishati inayouwezesha kufanya haya: movement, excretion, respiration, reproduction, irritation, nutrition, growth.
Ni kama ambavyo sumaku ikigongwa kwa nyundo inapoteza nishati ya sumaku. Ni kama ambavyo flush ya kompyuta inapoteza data ikifomatiwa. Ni kama ambavyo kompyuta inapoteza program pale inaposhtuka kwa sababu ya umeme kukatika.
Programu, data na nishati ya sumaku haviendi mbinguni. Vinahama kwa mujibu wa kanuni zianazoongoza uhusiano uliopo kati ya maada na nishati, kama alivyoeleza Albert Eisntein katika mlinganyo wake huu: E=MC*C.
Miduara ya kibailojia, kijiolojia na kikemia (miduara ya bayojiokemia-biogeochemical cycles) kama vile mduara wa kabonidioksiadi (CO2), mduara wa nitrojeni dioksaidi (NO2), mduara wa Oksijeni (O2) na kadhalika, ni mifano hai kueleza jinsi protein za babu yako aliyekufa zinavyoingia kwenye mimea, ukala mimea na kupokea protein hiyo mwilini mwako. Matter is neither created nor destroyed.
Kwa hiyo habari ya kwenda "mbinguni" inaweza kuwa na maana moja tu: nishati kuingia katika miduara ya bayojiokemia kuanzia mwilini mwako, kwenye miamba, kwenye mimea, angani na kisha kurudi kwenye mwili wako. Kama mbingu inayoongelewa ni anga, nakubaliana na hoja ya "roho kwenda mbinguni."
Mchana mwema.