ULIMWENGU WA ROHO: Nini hasa maana halisi ya kitu hiki?

Nimepata kitu hapo mkuu Mshana jnr. Ahsante sana
 
Ahsante sana kwa maelezo ya kina mkuu, ila naomba unisaidie kujua hasa unaposema wakristo wanahangaika na Roho badala ya mwili. Je, ni kweli kwamba wakristo HAWASHUGHULISHWI na mwili? Na je, nafsi nayo inaenda wapi baada ya Kifo?
Ahsante.
 
Ahsante, lkn hapa [emoji116]umesema;

"""Kama Kweli umedhamiria unataka kujua basi wenzetu Walio ktk ulimwengu wa roho watakusaidia na huyo ni cause and effect law."""


Walio katika Ulimwengu wa roho wako wapi? Ni kina nani? Nawapataje?

Msaada hapo [emoji115]tafadhali.
 
Mkuu Sued, ahsante kwa majibu yako mazuri yaliyojaa falsafa kwa sehemu nimekuelewa ingawa hapo uliposema ''waota ndoto ni washirikina! "
Nimejiuliza hapo, "je, wewe hujawahi kuota ndoto kweli? "
"Na je, ni kweli hata wale tunaoambiwa kwenye vitabu vya dini kuwa waliota/oteshwa ndoto nao walikuwa washirikina? "


Na hapa [emoji116]umenichekesha kweli, ati:

""" Kwa hiyo habari ya kwenda "mbinguni" inaweza kuwa na maana moja tu: nishati kuingia katika miduara ya bayojiokemia kuanzia mwilini mwako, kwenye miamba, kwenye mimea, angani na kisha kurudi kwenye mwili wako. Kama mbingu inayoongelewa ni anga, nakubaliana na hoja ya "roho kwenda mbinguni.""[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
.
Jawabu lipo. "Ulimwengu wa roho ni ulimwengu wa akili" iliyoko ubongoni mwako.
Kwa mujibu wa comment yako uliyomjibu Mshana jnr, umesema U NAKUBALIANA naye, lkn Mshana mwenyewe HAKUBALIANI na hicho umesema hapo juu!

Au unakubaliana na Mshana jnr wapi?
 
Mkuu kwa mbaaali nimejaribu kukuelewa ijapokuwa bado natatizika kwenye eneo ulipo huo Ulimwengu na mtu anawasiliana nao kivipi hasa?
 
Oh umeongeza jambo jipya hapo mkuu, SILVER CORD!!!!

Na pia sijaelewa uliposema roho inaenda mbinguni na nafsi inaenda paradiso au kuzimu!

Kwa hiyo kuna mbinguni, lkn pia kuzimu na paradiso?

Naomba ufafanuzi zaidi mkuu.

Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…