Ulimwengu wa Roho nini? Uko wapi?

Ulimwengu wa Roho nini? Uko wapi?

Kuna kitu kinanitatiza sana Wakuu?

Kuhusu hili swala la ulimwengu wa roho.
Je ulimwengu huo upo? Una utawala Kama ulimwengu huu?

Je unaweza kwenda na kurudi Huku?

Je ulimwengu huu ni wa mtu binafsi au wa wote?

Na kama ikitokea mtu amekutembelea katika himaya yako kwenye ulimwengu wa roho, je ni sahihi?

Je ni sahihi watu kwenda na kutembeleana katika ulimwengu wa roho ?

Je tulivyoumbwa tulielekezwa tuishi wapi, huu ulimwengu tuliopo au ulimwengu wa roho?

Je huo ulimwengu wa roho uko ndani ya Dunia hii au Dunia hii iko ndani ya ulimwengu wa Roho?

Kuna umuhimu wa kuufahamu ulimwengu wa roho?

Naomba kufahamishwa zaidi Maana nimesikia watu wengi wanauzungumzia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nfi ulimwengu wa roho upo mpaka kuuelewa ni lazima uingie uko ambao nao umegawanyika katika sehemu mbili kama wachangiaji walio pita wameeleza kua ni ule wa nuru na wagiza zipo njia nyingi za kuingia uko ila inategemea ni aina gani ya ulimwengu wa roho mfano wapo watu umu wanafundisha namna ya kutoka nje ya mwili soma huko na ujaribu kuingia katika ulimwengu mchafu ila ukipenda kuingia katika ulimwengu wa roho wa nuru liitie jina la Yesu mwamini nawe utaingia uko
 
Si vyema kusema hili swali ni gumu. Ila kabla ya kulijibu ni lazima wakati mwingine udadavue kujua kiini cha muuliza swali. Kitu cha kwanza msingi ni kuelewa maana na kwanini kuna ulimwengu wa Roho. Maswali mengine yote yatajijibu pindi mtu akielewa maana ya ulimwengu wa roho.

Kwa vile mimi ni mkiristo na kwa uelewa wa imani yangu napenda kusaidia kujibu maswali hayo katika hali yangu ya ukristo. Wote tunakubaliana kuwa kila mmoja wetu anayo roho (nafsi hai) ambayo iko ndani yetu. Nafsi hii imeshikana na mwili na vinategemeana. Na ndiyo maana wakati mtu anafariki nafsi ujitengana na mwili na ndipo mauti yanapomkuta mtu. Swali la kujiuliza je hiyo nafsi inayomtoka inakwenda wapi?

Kwenye kitabu cha Mwanzo1:26 biblia inasema (Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi). Katika mstari huu unatupa picha kuwa Mungu hapo mwanzo alimuumba mwanadamu kwa mfano wake na kwa sura yake, na kwa vile Mungu ni Roho hii ina maana hata sisi ni Roho kama alivyo Mungu.

Kama ambavyo nafsi iliyomo ndani yetu isivyoonekana lakini inatuongoza ndivyo Mungu wetu alivyo pia hatuwezi kumwona kwa macho ya nyama. Kuna wakati roho (nafsi) iliyopo ndani yetu inaongea, mfano kuna wakati unaweza kuwa umekaa lakini ghafla ukasikia sauti inaongea ndani ya moyo wako, sauti usiyojua imetoka wapi lakini inayokupa wakati mwingine majibu ya maswali yanayozunguka ndani ya kichwa chako.

Au kuna wakati unaweza kuwa unatembea wakati hauna hili na hili ghafla unasikia kama sauti inaongea ndani ya moyo wako unajiuliza kunani na wakati mwingine unaweza kusimama na kucheka tu mwenyewe ukabaki unajiuliza ulikuwa unaongea na nani? Jua kuna ulimwengu nje ya ulimwengu huu tunaouona kwa macho.

Mwanzo 2:7 (Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.) Ukiangalia huu mstari utangundua Mungu alitaka kiwepo kiumbe kinachoonekana kitakacho vitunza vitu alivyokuwa ameviumba ulivyokuwa vinaonekana katika ulimwengu wa macho ya nyama (haya macho tuliyo nayo). Mwanadamu aliyekuwa ameumbwa kwa mfano wake alikuwa katika roho hivyo asingeonekana kwa viumbe vyenye nyama. Kwa sababu hiyo ndiyo maana ilibidi Mungu amtengeneze mtu kutoka katika mavumbi (udongo) ambaye ataonekana katika ulimwengu wa nyama kisha akaipulizia ile Roho (mfano wake na sura yake) ikamwingia mtu kisha huyo mtu (udongo) ukawa nafsi hai. Kwa maana Roho kutoka kwa Mungu ikaungana na mwili vikawa kitu kimoja chenye uhai.

Sasa narudi kwenye swali lako ulimwengu wa Roho ni nini? na je Upo? Ulimwengue wa Roho ni maisha nje na mfumo wetu huu ambao tunaishi katika hali ya mwili na nyama, maisha yale ambayo macho yetu yanauona nje ya hapo ni mfumo mwingine ambao roho inaishi na huu ndo ulimwengu wa Roho. Ni kweli ulimwengu wa roho upo na ndipo yalipo makazi ya kila kiumbe kilichoubwa kuwa roho.

Ubarikiwe kama maelezo haya yatasaidia kujibu baadhi ya maswali yako.
Ahsante kwa maelezo yako mkuu lkn nina swali hivi nafsi na roho ni kitu kimoja hichi kitu huwa nashindwa kuelewa.
 
watu wadini mmeshindwa kumjibu mtu huyu? tuwaeleweje na hizo imani zenu..?
Hatujashindwa kumjibu. Tunaogopa mpu..uzi mmoja humu anaitwa MGEN huwa akikashfu uislam huwa anatoa picha watu wameinama msikitini kisha mwanaume mwingine anaonekana anamwingilia mwanaume mwenzie anayeswali humo msikitini.
Kiukweli ukiitazama vizuri hiyo picha inaonekana imepachikwa yaani huyo anayeonekana yuko nyuma mata.koni kwa mwenzie si halisi na wala haina uhusiano na mahala hapo. Sasa kwa upuuzi wa aina hiyo mjadala hauwezi kunoga maana kunakuwa na maneno ya uongo.
Isitoshe maandiko ya uongo kusingizia ni biblia au Quran ni kero sana JF.
Kama mtu ameshindwa hoja kwa nini asikubali tu? Kwani ukikiri ukweli utakufa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watakujibu vema kabisa
[HASHTAG]#mshana jr, [/HASHTAG] [HASHTAG]#divine[/HASHTAG] , [HASHTAG]#heavensent[/HASHTAG]
Ngoja waje mkuu
 
Si vyema kusema hili swali ni gumu. Ila kabla ya kulijibu ni lazima wakati mwingine udadavue kujua kiini cha muuliza swali. Kitu cha kwanza msingi ni kuelewa maana na kwanini kuna ulimwengu wa Roho. Maswali mengine yote yatajijibu pindi mtu akielewa maana ya ulimwengu wa roho.

Kwa vile mimi ni mkiristo na kwa uelewa wa imani yangu napenda kusaidia kujibu maswali hayo katika hali yangu ya ukristo. Wote tunakubaliana kuwa kila mmoja wetu anayo roho (nafsi hai) ambayo iko ndani yetu. Nafsi hii imeshikana na mwili na vinategemeana. Na ndiyo maana wakati mtu anafariki nafsi ujitengana na mwili na ndipo mauti yanapomkuta mtu. Swali la kujiuliza je hiyo nafsi inayomtoka inakwenda wapi?

Kwenye kitabu cha Mwanzo1:26 biblia inasema (Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi). Katika mstari huu unatupa picha kuwa Mungu hapo mwanzo alimuumba mwanadamu kwa mfano wake na kwa sura yake, na kwa vile Mungu ni Roho hii ina maana hata sisi ni Roho kama alivyo Mungu.

Kama ambavyo nafsi iliyomo ndani yetu isivyoonekana lakini inatuongoza ndivyo Mungu wetu alivyo pia hatuwezi kumwona kwa macho ya nyama. Kuna wakati roho (nafsi) iliyopo ndani yetu inaongea, mfano kuna wakati unaweza kuwa umekaa lakini ghafla ukasikia sauti inaongea ndani ya moyo wako, sauti usiyojua imetoka wapi lakini inayokupa wakati mwingine majibu ya maswali yanayozunguka ndani ya kichwa chako.

Au kuna wakati unaweza kuwa unatembea wakati hauna hili na hili ghafla unasikia kama sauti inaongea ndani ya moyo wako unajiuliza kunani na wakati mwingine unaweza kusimama na kucheka tu mwenyewe ukabaki unajiuliza ulikuwa unaongea na nani? Jua kuna ulimwengu nje ya ulimwengu huu tunaouona kwa macho.

Mwanzo 2:7 (Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.) Ukiangalia huu mstari utangundua Mungu alitaka kiwepo kiumbe kinachoonekana kitakacho vitunza vitu alivyokuwa ameviumba ulivyokuwa vinaonekana katika ulimwengu wa macho ya nyama (haya macho tuliyo nayo). Mwanadamu aliyekuwa ameumbwa kwa mfano wake alikuwa katika roho hivyo asingeonekana kwa viumbe vyenye nyama. Kwa sababu hiyo ndiyo maana ilibidi Mungu amtengeneze mtu kutoka katika mavumbi (udongo) ambaye ataonekana katika ulimwengu wa nyama kisha akaipulizia ile Roho (mfano wake na sura yake) ikamwingia mtu kisha huyo mtu (udongo) ukawa nafsi hai. Kwa maana Roho kutoka kwa Mungu ikaungana na mwili vikawa kitu kimoja chenye uhai.

Sasa narudi kwenye swali lako ulimwengu wa Roho ni nini? na je Upo? Ulimwengue wa Roho ni maisha nje na mfumo wetu huu ambao tunaishi katika hali ya mwili na nyama, maisha yale ambayo macho yetu yanauona nje ya hapo ni mfumo mwingine ambao roho inaishi na huu ndo ulimwengu wa Roho. Ni kweli ulimwengu wa roho upo na ndipo yalipo makazi ya kila kiumbe kilichoubwa kuwa roho.

Ubarikiwe kama maelezo haya yatasaidia kujibu baadhi ya maswali yako.
Kwa hiyohilo andiko linalosema Mungu alipomuumba mtu akampulizia pumzi linapingana na lile linalosema Mungu akikiamuru kitu kuwa basi huwa....?
Kun faya kun....!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kinanitatiza sana Wakuu?

Kuhusu hili swala la ulimwengu wa roho.
Je ulimwengu huo upo? Una utawala Kama ulimwengu huu?

Je unaweza kwenda na kurudi Huku?

Je ulimwengu huu ni wa mtu binafsi au wa wote?

Na kama ikitokea mtu amekutembelea katika himaya yako kwenye ulimwengu wa roho, je ni sahihi?

Je ni sahihi watu kwenda na kutembeleana katika ulimwengu wa roho ?

Je tulivyoumbwa tulielekezwa tuishi wapi, huu ulimwengu tuliopo au ulimwengu wa roho?

Je huo ulimwengu wa roho uko ndani ya Dunia hii au Dunia hii iko ndani ya ulimwengu wa Roho?

Kuna umuhimu wa kuufahamu ulimwengu wa roho?

Naomba kufahamishwa zaidi Maana nimesikia watu wengi wanauzungumzia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una amini mtu anakufa???

Kama ndiyo jiulize kifo cha mtu husababishwa na nini?

Ukimkagua kila kiungo utakikuta ila mtu huyo hayupo hai tena..! Ukipata majibu ya haya maswali utakuwa umeelewa kwa asilimia 70%.
 
Ulimwengu wa roho ndio sorce wa kila kitu unachokiona hapa duniani ulimwengu wa roho hauonekani kwa macho ya nyama ulimwengu wa roho kila kitu kinacho patikana huko ni roho ukiona gari huko ujue ni roho imegeuka kuwa gari umbali kutoka ulimwengu wa mwili hadi ulimwengu wa roho ni zero distance pia katika ulimwengu wa roho kuna sheria mbili tu zina tumika huko tena ulimwengu wa roho umegawanyika katika sehemu kuu mbili ulimwengu wa nuru na ulimwengu wa giza hivyo unaweza jikuta umetumbukia katika sehemu moja wapo nk ni raha sana ukizitumia sheria hizo hapa duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kuona gari ktk ulimwengu was roho imegeuka kuwa roho

Swali je Roho ni nini?
Mkuu kama umewahi kuota na katika kuota hko ukawa unaona kabs kuna kitu Unafanya ila c katika hali ya ulimwengu wa kawaida bs tambua huo ndo ulimwengu wa roho.
@>Ila kumbuka ziko limwengu za roho kama mbili, moja ulimwengu wa roho wachafu na mbili ulimwengu wa Roho watakatifu. Xx utatambuaje kuwa ww uko limwengu upi ni simple 2 kama unatabia ya kuota unakabwa, una sex, unakula, unakimbizwa, unapigana, unapaa, unaruka mito na mengineyo Ujue ww Roho yako Iko ulimwengu wa pepo wachafu
>kumbuka binadam anaishi limwengu mbili kwa wakati mmoja, binadam huyu anaishi dunian kupitia mwili na binadam huyu huyu anaishi ulimwengu usionekana au ulimwengu wa roho kwa kupitia ROHO yake.
>Ni mambo mengi ya kueleza ila kama ww ni mwelewa utakuwa japo nimekufumbua macho.
>Mwisho ulimwengu wa roho ni ulimwengu kamili ambao watu wa aina mbili huishi, moja wacha Mungu kweli ndo huishi katika ulimwengu wa roho mtakatifu, mbili watenda dhambi ambao nao wana ulimwengu wao wa waasi.
>Najua huamini ila utaamini zaidi cku ukifa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una amini mtu anakufa???

Kama ndiyo jiulize kifo cha mtu husababishwa na nini?

Ukimkagua kila kiungo utakikuta ila mtu huyo hayupo hai tena..! Ukipata majibu ya haya maswali utakuwa umeelewa kwa asilimia 70%.
Mtu ni roho inayo kaa ndani ya nyumba Nyumba inaitwa mwili roho ikitoka ndani ya mwili ndio tunasema mtu kafa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una amini mtu anakufa???

Kama ndiyo jiulize kifo cha mtu husababishwa na nini?

Ukimkagua kila kiungo utakikuta ila mtu huyo hayupo hai tena..! Ukipata majibu ya haya maswali utakuwa umeelewa kwa asilimia 70%.
Aaaa mkuu kifo cja mtu hisababishwa na malaria na magonjwa mengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wewe hata hujajua ulimwengu wa roho ni nini ila umejaza maswali ya kuhoji huo ulimwengu wa roho,sasa kama ukijakuambiwa kuwa huo ulimwengu wa roho huwa wanamaanisha nchi ya Marekani huoni kuwa hilo rundo la maswali yako yanakuwa hayana maana?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji115]

Sent from myself
 
Ahsante kwa maelezo yako mkuu lkn nina swali hivi nafsi na roho ni kitu kimoja hichi kitu huwa nashindwa kuelewa.
Nafsi na roho si kitu kimoja, kuna vitu vitatu hapa mwili, nafsi na roho
1. Mwili ni huu tulio nao, damu na nyama na maandiko matakatifu yanasema: mwili na damu havitaurithi ufalme wa Mungu. Inamaanisha wanaoishi kimwili pamoja na kutaka kuuridhisha mwili kwa matamanio yake yote.

2. Nafsi ni kitu ambacho ndani yake kuna mkusanyiko wa vitu vingi sana pamoja na akili, hisia, hasira, furaha, upendo, uchungu, kumbukumbu, chuki nk. Ndio maana wachawi wakitaka kummaliza mtu wanadili na nafsi, ili kumfanya aharibikiee kimaisha, watashika akili zake, ufahamu wake, hisia nk.
Hawawezi kudili na roho kwa kuwa hawana uwezo nayo.

3. Sasa roho ni ile nguvu au uweza wa Mungu uliopo ndani yetu, ambao kila mtu anao ndani yake. Roho inaweza kuwa hai ndani ya mtu au inaweza kuwa imekufa ndani ya mtu. Roho IPO kati ya mwili na nafsi. Roho yako inapenda wewe umjue Mungu, umtafute, umche, umtumikie, nk. Ukiona hivyo basi ujue roho inakuhukumu ndani yako kuwa wewe ni mwenye dhambi na ivyo unamhitaji Mungu.

Mwili unapokuvuta kufanya mbambo yasiyofaa ( unapotamani) kinyume na mapenzi ya Mungu, kama roho yako ndani yako imekufa basi nafsi yako, yaani akili yako mawazo yako, dhamili yako, utashi wako nk. Vitakuwa upande wa mwili, yaani mwili pamoja na nafsi yako vitakuwa kinyume na mapenzi ya Mungu. Ila nafsi ikijaa sana mawazo ya roho basi hautafanya chochote ambacho ni kinyume na mapenzi ya Mungu.
Ila cha kuzingatia hapa ni kwamba roho niliyoizungumzia ni roho iliyo ndani ya mtu na siyo roho Mtakatifu wa Mungu anayekuja ndani ya roho zetu sisi baada ya kumpokea kristo kama bwana na mwokozi wetu.

Ahsante sana nimeelewa.
 
Back
Top Bottom