No, hawa jamaa kamwe hawataweza kuchukua hatua kama tunavyotaka kwa sababu ile centre au huduma zipatikanazo pale wao ndio wanaonekana wako peke yao. Kwa kifupi wateja hawana sehemu nyingine ya kwenda ndio maana wanafanya mchezo huu. Kama kungekuwa na shopping malls nyingi, basi wangelazimika kuwajibika. Labda nitoe mfano; Mie nikienda dukani, customer care ikawa yakipuuzi au nikagundua nimeibiwa, basi duka hilo sikanyagi tena. Na hiyo haiishi hapo na waambie na wengine lililotokea na wao wataamua au kuchukua tahadhari. Vivyohivyo, mlimani city wanaamini watu kwenda pale hawana choice, wataibiwa na kurudi. Kwa sasa hivi nashauri tusemee saana tusichoke, lakini pia kama kuna uwezekano wa kupata huduma sehem ambazo ni salama twende huko tuone kama hawatarekebisha hali hii. Na tukilazimika kwenda pale, basi, tuhakikishe usalama wa mali zetu ni wa hali ya juu sisi wenyewe. Kwa maana wao wanashindwa hata kuweka CCTV kukawa na watu 2-3 wanaoperate na ingekuwa rahisi kuone wizi unapotendeka.