Ulinzi na kamatakamata UDSM leo

Mpambanaji K

Member
Joined
Dec 29, 2008
Posts
84
Reaction score
6
Serikali,imetangaza kimya kimya hali ya hatari UDSM. Hakuna mtu asiye mwanafunzi au mwalimu anayeruhusiwa kuingia chuo. maaskari wenye silaha wenye uniform na mashushu wako kila mahali. ndani ya chuo imekuwa kama barracks

Gharama ya kuweka hawa maaskari UDSM ni shillingi milioni mia(100,000,000). Maaskari wameninong'oneza kuwa wana amri ya ''kushoot na kuua''

Habari ndio hiyo


mp
 
Last edited by a moderator:
ya kweli haya? millioni 100 hata mimi nilisikia.
 
Siamini 100M inaweza kutumika kwa ajili hiyo lakini siwezi sema, mimi si kiongozi wala policy maker; Ila sipendelei Tanzania kuwa maarufu kwa Haya Ya kutumia excessive force sehemu isiyostahili... watoto wa shule wafikiriwe kama wanetu na si majambazi

Kuna siku viongozi wa sasa watawekwa panapostahili mbele ya haki... Duniani au akhera!
 
Askari mmoja ana gharimu kiasi gani kwa kazi maalumu? Posho yake na gharama za mabomu ya machozi

Gharama za utawala ni kiasi gani,ikiwemo vikao vya kupanga jinsi ya askari hao kugawanyika na kufanya kazi yao?

Watu wa usalama nao hulipwa bei gani kwa ajili ya kukaa vijiweni kunywa pombe kwa siku kwa lengo la kupeleleza?

Tukipiga mahesabu hayo tunaweza kujua ni askari wangapi wanahitajika ili kutumia milioni 100 na tunaweza kukadiria pana askari wangapi huko hivi sasa na hatimaye tutapata jibu kama habari hii ni ya kweli au imeongezewa chumvi

Kule kwetu Zanzibar waliwahi kumwagwa kwa maelfu, nadhani walitumia vijisenti vingi


Asha
 

Habari hii ina ushabiki wa hali ya juu sana, Watanzania acheni kuweka mbegu mbaya zisizokuwa na ulazima!

Ni upuuzi wa hali ya juu kusema serikali imeruhusu ku-shoot...
 

Mkuu Mpambanaji
Una uhakika na kauli zako?
 
Sipo Tanzania lakini hata mimi siwezi kulikubali bali kuna ushabiki usio wa lazima hapa, tujaribu kuandika vitu vyenye mantiki badala ya kutumia majukwaa murua kama haya kwa ushabiki usio na maana. kama kuna amri ya kutotaka watu kwenda kufanya fujo ni bora zaidi kwani wakizembea tutakuja hapa na lawama nyingine kuwa serikali ililiona lakini ikalizembea.
 
Sidhani kama ni ushabiki, ila kwa mimi ambaye nilijaribu ku-pitia njia ya Chuo Kikuu kwenda kazini, Naweza kuwahakikishia Ulinzi uiopo pale toka jana jioni ni zaidi ya George Bush alipotembelea State House - the only difference ni kwamba hakuna "Marines", otherwise ni hali zaidi ya state of emergency.

Nadhani ukijumlisha zile gharama zote kwa ufasaha 100m inaweza kufika
- tents
- posho za wadaili
- posho za maafisa usalama
- e.t.c
 
Watu inakuaje wanaona haiwezekani kutoa amri ya kushoot?? Kwani hii itakuwa ni mara ya kwanza TZ kufanya hivyo??? Si ni serikali hiyo hiyo ya CCM iliyotoa amri ya kushoot wakati ule wa mwembachai na kule Zanzibar, au siyo???? Mnataka mpaka watu wafe nidiyo muamini??? kama ni hivyo basi subirini kwani nyie mnataka kuwa mwanafunzi wa Yesu yule aliyeitwa Tomso.
 

Kama nimewaelewa vema waungwana hapo juu wanachotaka ni objectivity na kupunguza ushabiki katika kuelezea haya mambo. Kutoyaamini yanayoelezwa kunatokana na kuingiza ushabiki badala ya uhalisia
 
Kuna chanzo changu cha habari nimekiuliza pale Mlimani na kimesema huu ni uongo. Sasa kama wafanyakazi wamezuiwa, wale wanaofanya kazi za usajili wa wanafunzi ni akina nani? Baada ya kuanza na process za getini, wanafunzi wanaelekea kukamilisha usajili kwa wakuu wa vitivo vyao, sasa kama wanafunzi wanazuiwa, si wangejaa getini? Zile shuttle zinazofanya route za ndani zinabeba akina nani? Uongo mtupu!! Naendelea kuwasiliana na jamaa pale Mlimani, nitarudi. Lakini pamoja na mabaya waliyofanyiwa wanafunzi, tuwe tunasema ukweli, si kuweka ushabiki hapa.
 
Last edited:

Opaque: Mbona huonyeshi kama umewasiliana already au hukupata chochote ulipowasiliana; au ndio unaanza; sasa sema unaanza kuwasiliana na sasa tunasubiria output yako maana uliyoeleza hapa hayajazi kibaba
Mie niwe mkweli; Watanzania sasa ni kama manayang'au; yamejigawa kwa kutumia vijipesa tena vya muda; asiyenacho atapigwa risasi; ingawa kinachompeleka pale ni ELIMU; inaniuma sana; mtu na usongo wake wa shule leo hii anapigwa risasi; anaandaliwa jeshi sifike darasani; NYERERE kama angefufuka leo hii hakika angeanzisha chama kipya cha ukombozi dhidi ya mkoloni mweusi
 
Last edited:

Hebu tuonyeshe hapa kama kuna mtu ameandika kuwa wafanyakazi na wanafunzi wamekatazwa kuingia. Au mwenzetu unasoma kinyume nyume?

.....ndiyohiyo
 
Habari hii ina ushabiki wa hali ya juu sana, Watanzania acheni kuweka mbegu mbaya zisizokuwa na ulazima!

Ni upuuzi wa hali ya juu kusema serikali imeruhusu ku-shoot...



Kinacho kushangaza wewe ni kipi katika hilo ?Ndugu inaonesha kuwa wewe ni mwepesi wa kusahau kule zanzibar kwani si walifanya kama hivyo unavyihisi wewe au kuona ajabu (shoot)
 
Hebu tuonyeshe hapa kama kuna mtu ameandika kuwa wafanyakazi na wanafunzi wamekatazwa kuingia. Au mwenzetu unasoma kinyume nyume?

.....ndiyohiyo


Ni hapa...


Maaskari si walimu, wapo ndani. Benki zote zinafanya kazi, waajiriwa si walimu, dispensary iko wazi, manesi na madaktari si walimu, etc etc...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…