Ulinzi na kamatakamata UDSM leo


Mimi sipendi ushabiki ila siwezi kubisha kama hayo yaliyosemwa ni kweli. Maana hadhari iliyotolewa jana can easily lead to that. No surprises for me. After all, it's not the first time "to shoot and kill". Katika nchi yetu, "anything goes".
 
 

Wewe umesema hapa kuwa kuna mtu amesema kuwa Wanafunzi na Wafanyakazi wa chuo wamezuiwa. Kwenye utetezi wako umegeuza kauli sasa unazungumzia polisi na manesi. Hebu tuonyeshe mahali mtu amesema wanafunzi wameuzuia

....ndiyohiyo
 
Ffu wametambaa mpaka sinza na sehemu zingine ambazo kuna wanafunzi walikuwa wanaishi kwa wingi kama ubungo
 
 
 
Hivi mapesa yote haya wanayotumia kufanya udahili upya, kuweka ulinzi (silaha, magari, askari nk), vikao, publicity etc wanayatoa wapi? Ni ya walipa kodi au wafadhili? hayo mapesa si yangeweza kukopeshwa kwa wanafunzi kadhaa kulipia ada? Kwa maoni yangu haya ni matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za taifa. Na mbaya zaidi haya yanatokea chuo kikuu!
 
 
Hii serikali imeshindwa kupeleka hao FFU kusaka wauaji wa ALBINO wanapoteza hela bure kutisha vijana wa masikini
 
Wananfunzi wanne wako mikononi mwa polisi kwa kuchochea ghasia
 
Habari hii ina ushabiki wa hali ya juu sana, Watanzania acheni kuweka mbegu mbaya zisizokuwa na ulazima!

Ni upuuzi wa hali ya juu kusema serikali imeruhusu ku-shoot...

sio upuuzi au ushabiki ndugu. kama ungekuwa na muda ungepita chuo na ungejionea mwenyewe, na ungekuwa kama waaminio na siyo wasioamini.
na huwezi kuamini nguvu kubwa ambayo ipo pale. hata hizo gharama huenda zikazidi.
labda ni kusahihisha tu kuwa pale getini lazima useme unaenda wapi na uwe na kitambulisho bila hivyo huruhusiwi kupita! hivyo wafanyakazi wa chuo/benki/hospitali/ cafeteria ndani ya campus wapo kazini ila wamenyanyasika sana kwani asubuhi walipanga foleni kubwa sana na kunawatu wamezungushwa kwa zaidi ya saa mbili. mf mtu wa changanyikeni alizunguka msewe/rombo/ubungo/ na kurudi chuo nk.
Suala la kuua linategemea na resistance iliyopo, sasa sijui watu wanashangaa nini, mbona mara nyingi polisi/FFU wameua??
 
Hao FFU na bunduki zao wanalinda nini hasa ?
Kuna mgodi wa MADINI hapo UDSM?
 

Okay, asante kwa kuliweka hilo sawa sawa.

Currently Active Users Viewing This Thread: 53 (15 members and 38 guests)

Nadhani panahitajika information sahihi na ambazo ziko updated kwani kuna wengi tu wanafuatilia kutaka kinachoendelea pale UDSM. Mliopo maeneo ya huko endeleeni kutuhabarisha!
 
Waliokamatwa ni Issah Paul, Titus Ndullah, Sabinian Prinspius na Bahati Alone. Kamanda wa Kinodnoni, Kalunguyeye (nadhani ndio jina lake) amesema watafikishwa mahakamani kwa uchochezi
 
Nao wamezidii watulie warudi chuoni...wajipange upya kwa hoja this time sio nguvu tenaa.........wanatukera sana kasiiiutumia nguvu dhidi serikali......hawataweza...wajipange upya kuja ki sera ba
 
Kaongezeka mmoja huyo katoa lugha ya matusi wakati wa kudahiliwa kwa hiyo wapo 5 mahabusu.
 
 
Wana JF,

Inwezekana ni kweli habari hii imetiwa chumvi lakini kuna ukweli asilimia 90. Suala la kujiuliza ni kwa manufaa ya nani nguvu zote hizo zinatumika? Kuwazuia wanafunzi ambao hawakujaza form na kutimiza masharti? Kuna haja ya kutumia FFU na vitambaa vyekundu? Je ni kwanini DARUSO imefutwa wakati huu ambao wanafunzi walikuwa labda wanaihitaji zaidi ya wakati mwingine wowote. Je hii ni dalili ya utawala bora pale chuoni? Je hao askari watakaa hapo mpaka lini?

Hata wakiweka askari 5,000 ukweli unabaki pale pale kwamba serikali imeshindwa kupata njia sahihi ya kuendesha vyuo vikuu na ni aibu kubwa kwa Prof. Mkandala ambaye wengi tulikuwa tunamuheshimu na kumuona kama mwana mapinduzi halisi. Nashindwa kuamini ni yeye anayeruhusu haya yafanyike.

Time will tell!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…