Hodi na Saalam nyingi kwenu wanaJukuwaa
Nomabe niwakumbushe tena kwamba kumekuwepo na ongezeko la matukio ya wizi na ujambazi maeneo mbalimbali katika nchi yetu, hasa mijini. Matukio haya yanahusu uharibifu au wizi wa mali lakini pia watu kujeruhiwa na wengine kuuwawa.
Jitihada za Jeshi la Polisi ama kwa hakika haziridhishi na hazitoshelezi hata kidogo. Hata pale wanapopewa taarifa au kuitwa kwenye eneo la tukio wanakuja kwa kuchelewa sana na hivyo msaada wao unakuwa hauna tija tena. Usiniulize sababu, mpaka sasa naendelea kutafiti ili nibaini sababu!
Kutokana na hali hiyo basi ni dhahiri ulinzi na usalama wetu ni jukumu la kila mmoja wetu ktk ngazi yake yake na familia yake. Na kila mmoja wetu akiwajibika basi jamii na taifa itakuwa salama, naamini.
Mimi nimeanza utekelezaji huu kwa vitendo na kupitia jukwaa hili zaidi ya kutoa tahadhari hii ila pia naomba niseme nahitaji huduma ya kampuni ya ulinzi, maeneo ya chang'ombe keko, mlinzi mmoja asiye na silaha ya moto, kwa usiku tu kuanzia saa 12,00 jioni hadi saa 12,30 asubuhi, kila siku.
Kama una kampuni au unamfahamu mwenye kampuni tafadhali awasiliane nami kwa kupitia namba ya simu 0655 999 884 au baruapepe [email protected]
Nimeamua kuweka habari hii ktk jukwaa hili nikiamini kwamba swala la usalama na ulinzi wetu ni agenda kubwa kabisa ya siasa lakini pia kwa sababu jukwaa hili huwa nalitembea mara nyingi na bila shaka wengine pia wanatembea.
Asanteni sana.