Nasema Uongo Ndugu Zangu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 279
- 779
Katika mambo ya kipuuzi ambayo jeshi letu la polisi linayafanya ni hiki kitu kinaitwa ulinzi shirikikishi.
Sote tunajua maisha ya watanzania yalivyo, unakuta kijana anayejishughulisha na shughuli za kilimo jioni anarudi nyumbani hoi halafu unamtaka aingie mtaani eti kufanya doria ili kukomesha matukio ya uhalifu.
Kumbuka kuwa hana mafunzo yoyote ya kujihami, hana silaha ya maana zaidi ya zile za jadi na tochi matokeo yake ikitokea vijana hawa wamekutana na raia aliyelewa wanampiga na kujisifu kuwa wamepiga kibaka.
Sulala la usalama wa raia na mali zake ni jukumu la jeshi la polisi Tanzania, kama vile suala la ulinzi wa mipaka lilivyo chini ya jeshi letu la wananchi.
Haiwezekani tulipwe mishahara na serikali halafu tuwasumbue watu kutusaidia majukumu yetu.
Ipo siku vikundi hivi vya ulinzi vitakitana na wahalifu wenye silaha za moto na kwakuwa havina mafunzo vitapelekewa moto mpaka vikiambiwa viseme ubwabwa vinasema Wawa.
Nashauri serikali iajiri askari wakutosha tuachane na hii biashara haramu ya kuwasumbua watu usiku, tuwaache wapumzike baada ya mikiki mikiki ya utafutaji.
Tunawachukulia kodi, tunachukua tozo, tumeshindwa kuwasaidia kudhibiti mfumuko wa bei bado tunataka kuwaibia muda wao na ku risk maisha yao?
Hii ni dhambi Nasema Uongo Ndugu Zangu?