ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Katika vitu tumepigwa ni kufuli yaani kuliamini kufuli kwamba linalinda ni chai mchana kweupe ni ulinzi wa kizamani mno.kwanza kidude kinacholock ni kidogo sana yaani hata likipigwa na nondo linajifungua.pili kuna master key inafungua lock nyingi tu kwa hivyo padlocks sio kitu cha kukiamini hata kidogo kimekaa kisaikolojia zaidi kukuaminisha kwamba mlango wako uko salama ila kiukweli ni kwamba kufuli linapunguza tu uwizi ila mtu akikusudia ni linatekenywa kidogo tu linaachia.