Kumekuwa na matukio mengi ya kihalifu ambayo yanaongezeka kwa kasi hapa nchini.
Ubaya wa mtu na uzuri wa mtu upo ndani ya mtazamo wake, fikra zake.
Matokeo yote tunayo yaona katika nyanja mbali mbali ni zao la fikra.
Fikra zinaumba!, Binaadamu alikuwepo kabla ya uwepo wa nyumba, magari n.k.
Kutokana na changamoto binaadamu alizo pitia aliona Kuna uhitaji wa kuwa na makazi ambayo yatamsitiri kakubiliana na hali ya Mazingira yanayo mzunguka!
kwa hivyo fikra ilitangulia kujenga nyumba ndani ya akili kabla haijatokea nyumba halisi inayo onekana na kushikika!.
Hii ndiyo maana ninasema fikra inaumba!.
watu hawazaliwi kuwa wahalifu! bali changamoto wanazopitia katika Maisha na Mazingira zinasababisha wao kufikiria kutafuta masuluhisho!.
Hapa kwenye kutafuta masuluhisho ndipo panapo hitajika mtu apakute akiwa katika hali ya maandalizi salama.
Mtu huwa hazaliwi na kukuta changamoto anazo takiwa kuzitatua yeye mwenyewe!
Wazazi na jamii ni wahusika wakubwa katika utatuzi wa kuziondoa changamoto zinazo wakabili wato.
Na jukumu la kumuandaa mtoto kifikra na mtazamo linaanzia mikononi mwao!
Wazazi na Jamii wakishirikiana katika malezi salama ya watoto na Kisha wakawajenga kimaadili,subira na imani ya hofu ya Mungu!
Matokeo yake ni kwamba watoto hao watakapo fikia umri wa kutatua changamoto zao watatembea katika msingi wa malezi, watatafuta masuluhisho salama na jamii itaishi kwa salama na amani bila uhalifu.
Lakini leo Wazazi na Jamii wanaacha watoto wajilee wenyewe kimaadili, Matokeo yake kunakuwa na uzalishaji mkubwa wa watu ambao hawakuandaliwa kuwa na fikra salama,ambao ndiyo wanaleta shida katika jamii.
Fikra na mtazamo ni sifa ya kimaumbile! ambayo inabadilishwa kulingana na hali ya wakati na mahitajio!
Wazazi na Jamii wasipo timiza wajibu wa kuwalea watoto, Mazingira na hali zitawalea! ikiwa hali na Mazingira ni mabaya watakuwa wabaya! kwa sababu ubaya wa mazingira na hali ndiyo inakuwa mwalimu wao!
Kuhamasisha watu kumiliki silaha kwa sababu ya kujilinda kamwe hakuto saidia kupunguza uhalifu! bali uhalifu na mauaji vitaongezeka! kwa sababu jamii mbovu Kisha uipe na silaha itakuwa ni kuongeza tatizo.
Biashara ya silaha inategemea Sana uovu ili ifanyike!
Sisi watanzania tunatakiwa kuwa makini na uhamasishaji wa umiliki wa silaha za moto.
Huwenda tukawa tunatengenezwa kuwa soko la wauza silaha.
Nimesikitishwa na taarifa ya huko Mwanza Kiongozi wa dini anaomba na wao wapewe silaha za kujilinda!.
Viongozi wa dini wanatakiwa waombe nafasi zaidi ya kuwezeshwa kufanikisha malezi ya watoto! siyo kuomba silaha.
Marekani wamewekeza katika kuuza silaha hadi kwa raia Matokeo yake kila siku tunasikia watu wakiuana kwa silaha hizo hizo.
I.G.P. SIRO, Silaha kubwa ya kuushinda uhalifu ni kuwekeza katika malezi ya watoto!
Shirikiana na Serekali na Viongozi wa dini kuweka mpango wa kitaifa juu ya malezi salama ya watoto, elimu ya maadili iwe ni elimu ya lazima!