Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Jana katika ufunguzi wa RNC convention, Donald J. Trump aliingia ukumbini kuwasalimia wanachama wa chama chake.
Ndani ya ukumbi walikuwemo wanafamilia wa Trump pamoja na mteule wake wa makamu Rais.
Nilichokiona ambacho kilikuwa tofauti ni wakati Trump anaingia ukumbini.
Security detail ya jana ilikuwa tofauti kabisa na ile ya Jumamosi kwenye ule mkutano wake wa hadhara alipopigwa risasi.
Head wa detail alikuwa ni yule yule wa siku zote.
Jana sikuona mdada hata mmoja. Niliziona njemba zilizoshiba mithili ya Brock Lesnar au NFL linebackers.
Trump inasemekana ni 6 “2 na ana uzito wa ratili 200+.
Wale wadada waliokuwepo siku ile kwenye detail yake walionekana kutokujua nini cha kufanya. Kuna mmoja alionekana kama vile alikuwa ni muoga.
Kuna mwingine alionekana akipata shida kuiweka silaha yake kwenye holster!
Wale wadada, kwa muonekano wao, walionekana kuwa na vimo vya chini ya futi 6. Labda 5 “4 au 5 “6.
Wadau wengi sana wamehoji kwa nini hao wadada walikuwepo kwenye inner detail ya ulinzi wa Trump.
Wapo watu wanaodai kuwa hao wadada ni matokeo ya agenda ya DEI.
Binafsi sina tatizo na jinsia yao madhali walifuzu mafunzo yale yale wanaopitia walinzi wa kiume.
Hapa kwetu tumeona Rais Samia ana walinzi wachache wa kike.
Sijui Kama likitokea la kutokea kama wataweza kuifanya kazi yao kwa weledi.
Kila nikiangalia walinzi wa viongozi wa mataifa mengine, mfano India, Israel, na Urusi, sijawahi kuona wanawake wakiwa kwenye inner detail.
Walinzi wa Narendra Modi, Vladimir Putin, na Benjamin Netanyahu, ukiwaangalia tu unapata ile meseji ya ‘Fcuk Around and Find Out’ 🤣.